Ni sababu zipi ziliwafanya hawa washindwe kufufua Viwanda?

Ni sababu zipi ziliwafanya hawa washindwe kufufua Viwanda?

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165

Mwijage, Kakunda wakiri kushindwa kufufua viwanda​

WEDNESDAY JUNE 23 2021​

Summary

Mawaziri wa zamani wa viwanda na biashara leo Jumatano Juni 23, 2021 wamekiri bungeni mjini Dodoma kuwa walishindwa kufufua viwanda.
By Habel Chidawali
More by this Author

Dodoma. Mawaziri wa zamani wa viwanda na biashara leo Jumatano Juni 23, 2021 wamekiri bungeni mjini Dodoma kuwa walishindwa kufufua viwanda.

Charles Mwijage ambaye ni mbunge wa Muleba Kaskazini na Joseph Kakunda (Sikonge) kwa nyakati tofauti wamewahi kuwa mawaziri wa wizara hiyo katika uongozi wa Serikali ya awamu ya tano.

Mwijage akichangia hotuba ya muswada wa fedha ameitaka Serikali kuachana na mpango wa kufufua viwanda kwani yeye alivishindwa.

"Mpango wa kufufua viwanda achaneni nao fikirieni vitu vipya, mimi nilijaribu katika wakati wangu lakini nilishindwa kwa hiyo msipoteze muda kufikiria ufufuaji wa viwanda," amesema Mwijage.

Wakati Mwijage akiendelea kuchangia, alisimama Kakunda kwa ajili ya kumpa taarifa ambapo mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu alimpa nafasi ya kuzungumza.

" Mwenyekiti nampa taarifa mzungumzaji (Mwijage) kuwa hata mimi nilijaribu kufufua kiwanda kule Lindi lakini nilishindwa, kwa hiyo mchango wake ni sahihi kabisa," amesema Kakunda.
 
Kazi ya serikali ni kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji
Yaani wawafanye wawekezaji ndio wakafufue hivyo viwanda na sio wao kama serikali
Hao mawaziri wako vizuri

Haha haa aa...
Hii nchi hii, mpaka yatoke masisiemu yaliyoishiwa mawazo ndio nchi yetu itapata maendeleo
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hii nchi ni kama viongozi wanavuta bangi,yaani waziri unajisifu kabisa kwamba ulishindwa kufufua viwanda!?
Ajabu sana,Hivi Bakheresa si yupo TZ,
Mo dewji si yupo TZ,
Kwanini hamuwafati Hawa big thinkers waisaidie serikali!ni Swala la kuwa na think tank tu,Hawa watu wanauzoefu na biashara na viwanda kuriko ma profesa waliojaa nadharia za biashara,ambazo hawajawahi hata kufungua genge,
Kwanini hatuwatumii watu kama Hawa?kiwanda kama General tyre,ningekuwa Mimi Raisi,hiki unamkabizi Bakheresa au Mo,unampa msaada,Ili akiendeleze.
Mo dewji anamshauri Raisi wa Afrika kusini kuhusu biashara,sisi hapa Shetani JPM,alimteka?Ili kumtisha.
 
Sasa mnatuchanganya wakuu mbona Kayafa kaacha Tanzania ya V-WONDER leo tena Tanzakiza sio ya V-WONDER

Alafu na Mama alikuwa anaimba nyimbo hiyo hiyo Leo kawa kimya Kama hajui.
 
Unafufua viwanda bila fedha !.Fedha nyingi zilipelekwa kujenga Chato,Kununua ndege,Kujenga SGR na Kujenga Bwawa la kuzalisha umeme,Kununua Viongozi wa upinzani.

Hayo yote yalizekana kwasababu fedha zilitengwa na kupelekwa huko.

General Tyre mitambo ipo,Mould za kupika tyres zipo,Majengo yapo,Soko lipo ambacho hakipo ni fedha .Huu ni mfano mmoja ukitembelea maeneo mengine kama viwanda vya kubangua korosho story ni hizo hizo hakuna fedha.

Ukitazama msafara wa Mwendazake kipindi cha uchafuzi mkuu utashangaa V8 zaidi ya 80 sasa huo kama si ufujaji ni nini ?.

Viongozi wa kiafrika ni tatizo kuu ambalo sioni siku tutakuja kulitatua.
 
Hii nchi ni kama viongozi wanavuta bangi,yaani waziri unajisifu kabisa kwamba ulishindwa kufufua viwanda!?
Ajabu sana,Hivi Bakheresa si yupo TZ,
Mo dewji si yupo TZ,
Kwanini hamuwafati Hawa big thinkers waisaidie serikali!ni Swala la kuwa na think tank tu,Hawa watu wanauzoefu na biashara na viwanda kuriko ma profesa waliojaa nadharia za biashara,ambazo hawajawahi hata kufungua genge,
Kwanini hatuwatumii watu kama Hawa?kiwanda kama General tyre,ningekuwa Mimi Raisi,hiki unamkabizi Bakheresa au Mo,unampa msaada,Ili akiendeleze.
Mo dewji anamshauri Raisi wa Afrika kusini kuhusu biashara,sisi hapa Shetani JPM,alimteka?Ili kumtisha.
Mkuu naongezea na baadhi ya viwanda
Tanganyika parks
Urafiki....
 
Hata Mama alikuwa sehemu ya utawala na aliyekuwa waziri wa fedha Leo ndo VP hawa wote wanapaswa kuwajibika kwa kudanganya Umma kuwa serikali inajenga v-wonder kila mkoa
 
Hata Mama alikuwa sehemu ya utawala na aliyekuwa waziri wa fedha Leo ndo VP hawa wote wanapaswa kuwajibika kwa kudanganya Umma kuwa serikali inajenga v-wonder kila mkoa
Hivi vile viwanda 10,000 kila mkoa tulivyoambiwa ndugu zangu vilijengwa au vilikuwa vile vya cherehani nne....
 
Jiwe alikuwa anataka kuwafanya watanzania wote kuwa wajinga, waoga na waongo. Kifo chake ndio kimeuumbua utawala wake katili na uliokuwa umejaa upuuzi mtupu.

Wapambe wake wamekuwa wakimkana hadharani kila siku.
 
Hivyo viwanda havijawahi kujiendesha kwa faida. Hata kipindi cha Nyerere vilikuwa ni kutufilisi tu.
 
Mwijage alikuwa kama mr. Bin kwenye wizara ya viwanda. Alikomaa na nadharia ya "cherehani 4 ni kiwanda"
 
Viwanda!mnataka kuwa tia njaa importers 😆

Ova
 
Yaani bure kabisa hawa Mkuu! Bungeni wanatamka kwamba walishindwa kufufua Viwanda, lakini sababu husika zilizowafanya kushindwa hawakuziweka hadharani. Tanzania ya VIWONDER. Na kwanini hawakusema walipokuwa Mawaziri!? Oh! Waliogopa KUTUMBULIWA na yule dhalimu.
Unafufua viwanda bila fedha !.Fedha nyingi zilipelekwa kujenga Chato,Kununua ndege,Kujenga SGR na Kujenga Bwawa la kuzalisha umeme,Kununua Viongozi wa upinzani.

Hayo yote yalizekana kwasababu fedha zilitengwa na kupelekwa huko.

General Tyre mitambo ipo,Mould za kupika tyres zipo,Majengo yapo,Soko lipo ambacho hakipo ni fedha .Huu ni mfano mmoja ukitembelea maeneo mengine kama viwanda vya kubangua korosho story ni hizo hizo hakuna fedha.

Ukitazama msafara wa Mwendazake kipindi cha uchafuzi mkuu utashangaa V8 zaidi ya 80 sasa huo kama si ufujaji ni nini ?.

Viongozi wa kiafrika ni tatizo kuu ambalo sioni siku tutakuja kulitatua.
 
Viwanda vina miundombinu na teknolojia ya zamani, kukifufua ni bora ujenge kipya
 
Back
Top Bottom