Kamawewe
JF-Expert Member
- Jan 16, 2013
- 533
- 521
Habari wana JF
Leo kupitia vyombo vya habari ikiwemo clouds fm wamedokeza matokeo ya tume iliyoundwa na Waziri mkuu kuhusu matokeo mabaya ya kidato cha nne. Baadhi ya mapungufu yaliyobainishwa na tume ni pamoja na
(1)Wanafunzi kupewa alama (marks) kwa kufanya maswali ambayo hayakwepo kabisa kwenye mtihani mzima wa somo husika (2) Wanafunzi kufanya mitihani hasa ya sayansi ambayo ilihitaji masaa sita badala ya masaa 3 au2 waliyopewa.
Zaidi ya hayo mimi binafsi ninafahamu yafuatayo
(1) Mtihani uliopita kuna wanafunzi waliowekewa alama katika masomo ambayo hawakufanya kabisa wala hawajawahi kusoma, akiwemo mtu wa karibu yangu.
(2) NECTA yenyewe ina uozo wa kuwabadilishia matokeo watu waliofeli ili waende vyuo vya ualimu, unesi n.k hii hutokea baada ya kupokea rushwa.
(3) Watu wenye ushawishi NECTA ikiwemo management hutumia vibaya fursa ya ku appeal dhidi ya matokeo mabaya ya mitihani
(4) NECTA kuna rushwa sana
Ninachukua fursa hii kusema Ndalichako asirudi tena NECTA hafai, ebu tujaribu Msomi mwingine na ninyi mnaemshabikia kama dini ebu acheni aende zake kwanza kuna watu wengi bora nchi hii hawajapata fursa.
Karibuni kwa mjadala