Ni sahihi Dr Ndalichako wa NECTA kuondoka, ameharibu

Ni sahihi Dr Ndalichako wa NECTA kuondoka, ameharibu

Kamawewe

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2013
Posts
533
Reaction score
521
Habari wana JF
Leo kupitia vyombo vya habari ikiwemo clouds fm wamedokeza matokeo ya tume iliyoundwa na Waziri mkuu kuhusu matokeo mabaya ya kidato cha nne. Baadhi ya mapungufu yaliyobainishwa na tume ni pamoja na
(1)Wanafunzi kupewa alama (marks) kwa kufanya maswali ambayo hayakwepo kabisa kwenye mtihani mzima wa somo husika (2) Wanafunzi kufanya mitihani hasa ya sayansi ambayo ilihitaji masaa sita badala ya masaa 3 au2 waliyopewa.

Zaidi ya hayo mimi binafsi ninafahamu yafuatayo
(1) Mtihani uliopita kuna wanafunzi waliowekewa alama katika masomo ambayo hawakufanya kabisa wala hawajawahi kusoma, akiwemo mtu wa karibu yangu.
(2) NECTA yenyewe ina uozo wa kuwabadilishia matokeo watu waliofeli ili waende vyuo vya ualimu, unesi n.k hii hutokea baada ya kupokea rushwa.
(3) Watu wenye ushawishi NECTA ikiwemo management hutumia vibaya fursa ya ku appeal dhidi ya matokeo mabaya ya mitihani
(4) NECTA kuna rushwa sana

Ninachukua fursa hii kusema Ndalichako asirudi tena NECTA hafai, ebu tujaribu Msomi mwingine na ninyi mnaemshabikia kama dini ebu acheni aende zake kwanza kuna watu wengi bora nchi hii hawajapata fursa.
Karibuni kwa mjadala
 
Umetoa hoja nzuri kuhusu report na kwa nini mhusika hafai. Unachemka unaposema kama udini. . . Huhitaji kusema hayo kwani ukiingiza udini unadokeza pia kwamba inawezekana report imechakachulika kidini.
 
Ooh sorry mkuu hapa nimesema mnaemshabikia kama dini sikuwa na maana ya udini nilikuwa na maana wale wanaomshabikia Dr Ndalichako kama dini, kwa kuwa kawaida binadamu akiamini dini fulani daima hakubali ata akiambiwa dini yako ina mapungufu fulani, ninasema hivyo kwa sababu kuna watu wengi hawataki kukubali wala kusikia kwamba huyu mama amekosa uwajibikaji NECTA imeoza kwa hayo niliyoyataja.
Umetoa hoja nzuri kuhusu report na kwa nini mhusika hafai. Unachemka unaposema kama udini. . . Huhitaji kusema hayo kwani ukiingiza udini unadokeza pia kwamba inawezekana report imechakachulika kidini.
 
Vipi boss wa Ndalichako (Kawambwa), amafaa kuendelea au aachie ngazi?
 
Habari wana JF
Leo kupitia vyombo vya habari ikiwemo clouds fm wamedokeza matokeo ya tume iliyoundwa na Waziri mkuu kuhusu matokeo mabaya ya kidato cha nne. Baadhi ya mapungufu yaliyobainishwa na tume ni pamoja na
(1)Wanafunzi kupewa alama (marks) kwa kufanya maswali ambayo hayakwepo kabisa kwenye mtihani mzima wa somo husika (2) Wanafunzi kufanya mitihani hasa ya sayansi ambayo ilihitaji masaa sita badala ya masaa 3 au2 waliyopewa.

Ha ha ha ha, natamani ningeona hiyo karatasio ambapo mtu amejibu swali ambalo hakuulizwa na akapata alama. Kuhusu mitihani ya sayansi kuhitaji masaa 6 badaLA YA MAWILI AU MATATU WANAYOPEWA, MBONA WANAFUNZI WENGI WA SHULE ZENYE WALIMU NA VIFAA KAMA MZUMBE NA KIBAHA HUMALIZA MITIHANI HIYO KABLA HATA YA MASAA MATATU NA HUPATA A?
 
Wote ndio wale wale, ila kama wewe unategemea kujiunga chuo usihofu sana upande wa HESLB maana wame-reopen applications for loans, try to make a follow up.
Dah! Hapo patamu.... Kaka usizungmzie tu NECTA, gusia hata TCU;HESLB....
 
watu wa dini ya mtume mnatapatapa pelekeni watoto wenu shule nzuri watafaulu tu.
 
Ndalichako bado anafaa sana tena sana
Lakini fitna nchi hii zina nguvu sana
 
Ndalichako bado anafaa sana tena sana
Lakini fitna nchi hii zina nguvu sana

kwa kweli huyo mmama ctaki hta kuckia jna lake....ameharibu sna future za watu
akapumzike aachie wengine
mara zote mwisho wa ubaya
ni aibu,,aende salama wala asihusishwe tena
ktk taasisi yoyote ya serikali hpa tz.
 
Back
Top Bottom