Mimi Sioni ubaya wowote kubeba handbag ya mpenzi wangu, kama nisipo mfurahisha mpenzi wangu nikamfurahishe nani? Mimi Nabeba na wala sioni aibu kubeba handabag ya mpenzi wangu. Tatizo la sisi Waafrika hasa Watanganyika tumekuwa na kasumba ya kuona ukimsaidia mke wako au demu wako umelishwa libwata. Mtasema sana lakini sitowacha kumsaidia mke wangu au mpenzi wangu. Hata kupika huwa nitamwambia apumzike leo naingia mwenye jikoni zamu yangu, Mimi nakaa na demu wangu hata kushafisha nyumba weekend nasafisha. Unapokuwa na mke ndani usikirie una mtumwa bali ni mwenzako wa kusaidiana katika maisha na sio house girl.