Ni sahihi kuendelea kuwasiliana na Xboyfriends wakati umechumbiwa tayari?

Mcheza Karate

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2011
Posts
690
Reaction score
350
Habari zenu wadau? Poleni na mihangaiko ya kimaisha!


Wadau, wiki jana nilikuja na mada hapa jamvini kuwa mchumba angu hataki kutoa kitu hadi siku nikimwoa.

Lakini nimegundua kuwa anaendelea kuchart na wanaume wengine. Nilivyomuuliza anadai kuwa hao ni wapenzi wake wa zamani hivyo bado hajawaambia kuwa anaolewa lakini nisijali atawapotezea taratibu! Kwani hawezi kuwatosa ghafla.

Nahisi nimevunjika moyo kabisa na nimeamua bora nimpotezee kabisa huyu binti.

Kabla sijachukua uamuzi tofauti naomba ushauri wenu!

Nawasilisha!!!
 
Unabeba matatizo nyumbani mkuu...for sure haheshimu mahusiano yenu.
 
Ati atawapotezea taratibu??hapo tu ndo ameniacha hoi khaaa! POLE!
 
Hahahahahahahahahahaha, me nilikwambia lazima anampa mwingine, sasa umeamini! Kwanini akunyime wakati alishatoa mara nyingi tu?

Hongera kwa kutaka kufanya maamuzi magumu na sahihi, mwanamke akikunyima ina bidi ufanye uchunguzi.

Huyo mpotezeeeeeee usije ukaja na uzi wa mchozi jamvini.
Duuuuh,hapo ex-boyfriend anapewa wewe una subiri!

Kweli Old is Gold
 
tafakari mara ya pili jibu utakuwa nalo mwenyewe kaka
 
wachana na Valu valu , wewe unangojeshwa mpaka ndoa wakati si ajabu hao xboyfriends wanajimegea kiulaini.

Hafai kuoa huyo, tupa nje.
 
Hivi utawaitaje hao ni X wakati we mwenyewe currently hujaona king...mi nadhani wewe hapa ndio X...LOL
 
Hard to judge ila fanya unachoamini ni sahihi
 

ah! Kweli mkuu ni msumbufu kupitiliza na nadhani kuna kitu back the scene. Ahsante!
 
mmmh...! hapo kuna walakin kakangu. huyo dada atakua hajakupenda kwa dhati ila kwa kuwa wewe umemtakia 'ndoa' amejiona hana budi kukubali japo mapenz nawe hana. mimi ni msichana, kama ningekua kwenye situation kama hiyo (uchumba) nisingewatilia maanani hao Xs'bali ningeconcentrate na wewe. kwa hiyo kaka hapo naona kama ukioa utammiliki ng'ombe lkn wakamuaji maziwa watakua hao Xs'....!
 
Kwanini akukatalie wakati alishawagawia wengine...pili anaendelea kuchat nao hao ex, sijui ni wangapi katika list...tatu.. bado unajipa moyo kuwa utaawacha taratibu.

Wajua kuna jina maalum kwa watu design zenu.. ruttashobolwa atakwambia
 
Last edited by a moderator:
Ulimwengu wa mapenzi ni mgumu sana kuishi, hv inakuaje mtu umetoa maamuzi ya kuishi na mtu lakin bado unatoa nafasi kwa wanaume wasiokuwa na future na wewe? Hao ni watafunaji tu hawana lolote, tena kabla hujamega kapimeni huyo si mwaminifu kabisaa! Loh kimbia fasta mwache aendelee nao
 

Aisee kaka mtandao wako wa ngono umeunganishwa na Mr.President...Kumbuka:Malaysia ni nchi inayoongoza kwa kilimo cha mpira!
 
Kwa kifupi anakuchora au anakuchuna na amejaza nafasi ya mwanamke mwingine kwako.
mwache haraka ili wa kwako akija asikute hilo jini
 

Kabla ya yote, how old are you??

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
he he he he.

Inawezekana kabisa, labda anaolewa na wewe tu ila anapenda X's wake.

Kuna mtu mwingine unatamani kumpa, ila ukimuona tu apetaiti kwishney kabisa.
 
Second Hand haifai kabisa yani, ahaaaaa.....badala ya kutuliza kichwa .....anafanya comparison
hana maana
ingekuwa me ningeshamchinjia baharini
Shimo achimbe panya nyoka aishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…