Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari zenu wadau? Poleni na mihangaiko ya kimaisha!
Wadau, wiki jana nilikuja na mada hapa jamvini kuwa mchumba angu hataki kutoa kitu hadi siku nikimwoa.
Lakini nimegundua kuwa anaendelea kuchart na wanaume wengine. Nilivyomuuliza anadai kuwa hao ni wapenzi wake wa zamani hivyo bado hajawaambia kuwa anaolewa lakini nisijali atawapotezea taratibu! Kwani hawezi kuwatosa ghafla.
Nahisi nimevunjika moyo kabisa na nimeamua bora nimpotezee kabisa huyu binti.
Kabla sijachukua uamuzi tofauti naomba ushauri wenu!
Nawasilisha!!!