Ni sahihi kumpa ama kutompa maji ya kunywa mtoto mchanga chini ya miezi 6?

Ni sahihi kumpa ama kutompa maji ya kunywa mtoto mchanga chini ya miezi 6?

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Ni ushari unaotolewa katika mahospitali yetu lakini kuna dr Bingwa mmoja nilimsikia kwa masikio yangu akipinga suala hili la kutowapa maji watoto akidai marufuku.

Hiyo ililetwa kwa vile ilihofiwa watoto wangepewa maji yasiyo salama hasa maeneo yenye shida ya maji!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Je, ni salama kwa watoto wachanga kunywa maji?



Kunywa maji sana inaweza kuwa hatari kwa watoto wachanga.
Swali:

Je, ni salama kwa watoto wachanga kunywa maji?

Hata kama maji yakiwa ni salama ni hatari kwa watoto wachanga.

Katika kipindi cha miezi sita kabla ya kuanza vyakula imara, kiasi cha maji ambayo yapo katika maziwa ya mama au formula kawaida hutoa virutubisho vyote ikiwemo maji.

Maji mengi mno yanaweza kusababisha maji ulevi(intoxication) kwa watoto.

Lakini tofauti na watu wazima, ambao huwa na kupata sodium sana katika vyakula mbalimbali, watoto kwa kawaida hupata elektroliti wanazohitaji kutokana na maziwa ya mama .

Maji mengi kwao hupoteza sodium sana na kusababisha kuwashwa, ubongo kuvimba, pamoja kifafa.


Nini kuhusu maji mwilini?

Kama una wasiwasi kwamba mtoto wako kapoteza maji, wasiliana na mtoa huduma wako wa afya.

Tunatarajia watoto akojoe angalau mara moja katika masaa 24 ya kwanza ya maisha,

Mara mbili katika masaa 24 pili, na angalau mara tatu kila siku baada ya hapo.


Nini kuhusu vimelea na viumbe wengine katika maji ya kunywa?

Maji yanaweza kuwa na bacteria wanaosababisha magonjwa mbali mbali hivyo kuhatarisha afya ya mtoto.
 
Kwa mie maji ni mazuri sana kwa watoto. Mie nawapaga wanangu maji kidogo kidogo wakiwa wachanga wakate kiu. Na wanakua wakizoea maji na kuzidi kunywa zaidi wenyewe. Kwa wangu wamezoea maji na namshukuru Mungu yanawasaidia sana na kujenga immune system yao. Wanaweza kupambana na magonjwa wasiugue ugue kuwa hoi.

Maji ya kilimanjaro lazima yajae kwangu hata mmoja akinywa ma lita kwa siku sisikii uchungu wa pesa nazotumia maana naona matokeo yake. Mmoja aliumwaga malaria ile ya kulala na sindano juu bali duh alikuwa anacheza na dozi inaendelea.

Na kila siku nawahisi sana na kuwakumbushia maji nikiona wamecheza haswa wamekaa nawaambia kunyweni maji.

Najua hiyo ya kuambiwa na madaktari wengine ila na mie niliulizaga Dr akaniambia mpe mtoto maji( sasa wachanga wanatakiwa kunyywa maji ya kuchemsha yaliyopoa hadi wakifika mwaka mmoja ni muhimu sana kwa afya yao kujengeka). Mama yangu pia aliniambia maji mazuri kwa mtoto na nimejionea.

Nakueleza kwa yangu, ila ulezi mambo mengi na hisia ya mama mzazi uchangia vizuri kulea. Kwa mie ningekushauri mjaribishe kidogo kidogo uone kama inaleta tofauti na akitaka zaidi mpe atazoea ila usifanye ni mlo akiwa na njaa. Yaani mpe baada ya maziwa au kama kutokea kiu. Sio kumpa ukiona analia njaa hiyo hapana as atakuwa anajaza tumbo na maji tu na hapo hapati ya mlo.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Maji muhimu i have been giving water to my children since day one no side effects
 
Kijiko cha chai kimoja hadi vitatu tosha kabisa, lakini usisahau kuchemsha maji.
 
Back
Top Bottom