Ingawa Wataalamu wanaamini kuwa Maziwa ya Mama ni chaguo zuri kwa mtoto mchanga, kunyonyesha haiwezekani kwa kila mama mzazi.
Wengi wao maamuzi ya kunyonyesha au kutumia formula(maziwa ya kopo) yanategemea na life style, matibabu maalumu anayopata mama na pia comfort ya huyo mama.
Kwa wamama ambao hawawezi kunyonyesha au wameamua kuto nyonyesha, formula(maziwa ya kopo) ni mbadala mzuri, ina provide virutubisho vinavyomsaidia mtoto kukua na kustawi.
Baadhi ya kina mama wanahofia wasipo nyonyesha hawatakuwa na bond na watoto wao, ukweli ni kwamba upendo/mapenzi ya mama siku zote yatawaunganisha na watoto wao.
Ila katika kunyonyesha ndio muda mzuri wa kukuza Bond na mtoto.
Uamuzi wa kunyonyesha au kutumia formula(maziwa ya kopo) kwa watoto ni maamuzi binafsi,
Cha muhimu ni kupima faida na hasara za matumizi ya njia hizo mbili na kuamua njia ipi ni bora Kwako na kwa mtoto wako.