Ni Sahihi Kutumia Nondo za 10mm Kwenye Mifereji ya Paa la "Hidden Roof"?

Mimi nakushauri upaue kawaida, yaani hilo paa exposure to sunlight iko so close and direct, angalau hilo paa la kawaida kuna space kabla ya boards (gypsum). Kingine huwezi kuzuia maji yasishike kwenye kuta, so utahangaika sana
Water proofing material zimejaa siku hizi, sioni sababu ya kuogopa. Tatizo wabongo mnatembea sana na story za kusikia
 
Water proofing material zimejaa siku hizi, sioni sababu ya kuogopa. Tatizo wabongo mnatembea sana na story za kusikia
Exposure ndo tatizo .neno woter proof kwao ni mtihani achilia hivyo vingine
 
Kwani injinia aliye design jengo lako kasemaje? Maana yeye ndiye anajua nondo gani ya kuweka kwenye jengo na kwanini, hii sio kazi ya fundi wala sio yako.
 

Asipo elewa akatafte mganga kwa hii Nondo
 
Exposure ndo tatizo .neno woter proof kwao ni mtihani achilia hivyo vingine
Kabisa mkuu. Mtu anatoa comments tena kwa mihemko kabisa. Material kibao kwajili ya kazi kama hizi zimejaa madukani.
Nimepaua hii stail na sijawahi kuona hata tone la maji
 
Usanifu wa upauaji kisasa hauhitaji fundi njaa,,hauhitaji mbambamba katika materials hizi nyumba ni nzuri kwa muonekano lakini hazifai kuishi mosi nyingi huvuja pili hazina maisha marefu kwa sababu ya mzigo mkubwa inao ubeba juu hii hutegemea na msingi una huimara kiasi gani lakini tujifunze hizi nyumba zilikuwepo mwanzo tuliziita msumbiji leo zipo kwa kiasi gani unaweza kuzi renovate, kwanini zimerudi hapo hawali zilijengwa na mashirika Kama idara ya maji taasisi za kidini kampuni za kichina Kama temporary house ambazo huachwa baada ya kutumika mda mchache mfano zile za busisi usasa wake unatoka wapi..kifupi hizi nyumba hazijengwi na mlala hoi
 
Ni vizuri ukatumia nondo za 12mm kwa sababu kwenye kingo za huo mfereji (pembeni) kuna kozi ya tofali inapita, lakini pia sehemu ya uzito wa paa unaegemea kwenye huo ukuta wa kingo...tumia nondo za 12mm na wire mesh kwa usalama zaidi
 
Mi sijawahi kuwaamini wahandisi wa makaratasi kamwe
 
Ni vizuri ukatumia nondo za 12mm kwa sababu kwenye kingo za huo mfereji (pembeni) kuna kozi ya tofali inapita, lakini pia sehemu ya uzito wa paa unaegemea kwenye huo ukuta wa kingo...tumia nondo za 12mm na wire mesh kwa usalama zaidi
Paa kuegemea kwenye ukuta wa kingo inategemea namna mfereji ulivyowekwa.. kuna mifereji inakaa kwa nje na inayokaa kwa ndani ya nyumba.. inayokaa nje ya nyumba paa linaegemea kwenye ukuta wa nyumba.
 
Mi sijawahi kuwaamini wahandisi wa makaratasi kamwe
Inawezekana unachanganya kati ya Mafundi Mchundo na Wahandisi. Mafundi Mchundo (Technicians) hawa ndiyo mafundi wa kujenga, Wahandisi wao kazi yao si kujenga, bali kazi yao ni kuwasimamia mafundi mchundo kujenga kwa mujibu wa Ramani na kwa kufuata kanuni za ujenzi husika!!

Halafu ujenzi bora huanzia kwenye makaratasi.
 
Kazi ya technician sio kujenga ni kuimplement kile alichodizain engineer pamoja na kufata kanuni za ujenzi tofautisha Kati technician na Craftsman

Sent from my Pixel 3a using JamiiForums mobile app
 
Hidden Roof inahitaji ujuzi wa Engineering ndio akushauri ili kuondoa errors kwa ushauri njoo pm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…