Ni sahihi kutumia sabuni ya kuoshea vyombo kuongea?

Ni sahihi kutumia sabuni ya kuoshea vyombo kuongea?

Nimelishuhidia zaidi ya mara moja katika sehemu tofauti!

Kipande kimoja cha sabuni kinatumika kwa matumizi zaidi ya moja:
1. Kuoshea vyombo vya kupikia
2. Kuoshea vyombo vya chakula
3. Kuoshea vyombo vya kunywea maji
4. Kunawia mikono kabla na baada ya kula
5. Kuogea.

Kwa sababu sabuni iyo hiyo inatumika kwa matumizi yote hayo, kuoshea vyombo vya chakula na kuogea, ni kawaida kuikuta ikiwa na tunywele, hivyo muosha vyombo asipokuwa makini, unaweza kukutana na tunywele tudogo kwenye vyombo vya chakula.

Hilo limekuwa likinipa ukakasi.

Wengine mnalionaje? Ni kawaida au ni tabia ya uchafu?
Kuwa sahihi au kutokua sahihi inategemea na uwezo wako kiuchumi
 
Siyo kuogea tu na kazi nyingine ipo
 
Back
Top Bottom