Tone yako ipo rude, unadhani unajua kumbe hujui. Kuna uwezekano wa mambo mawili kuhusu tone yako:
1.Huna maarifa ya tafakuri tunduizi(Critical thinking skills)
2.Ni mjinga tu usiejua mambo
Ipo hivi, pamoja na kwamba utamaduni hutawala sana mambo mengi tufanyayo, hali hii isikutie ujinga na kufikiri kile unachofanya au ulichofunzwa tangu utoto ni sahihi kwa kila mtu. Yaweza kitu hiki kikawa sahihi au si sahihi kwako, lakini si kwa kila mtu.Kwahiyo, pamoja na kwamba utachukia, wakati wote ujifunze kukubali mawazo mbadala. Kuna baadhi ya vitu tunaweza kukubaliana bila shida, mathalani, kuzama na kuibuka kwa jua, kwani suala kama hili mnaweza kuthibitisha kisayansi.
Kuna baadhi ya mambo ni suala la mtazamo tu, mfano, uzuri na ubaya.Na hapa ndipo hoja yako inaingia.Uvaaji wa Kandambili au vazi lolote ni suala utamaduni na mitazamo tu, chochote kinawezekana.
Zingatia
Suala hapa si faida au hasara ya kuvaa kama baadhi wanavyotoka kwenye mjadala, suala ni uvaaji tu. Hayo ya faida ama hasara ni mada nyingine kwani hata vya kudumbukiza vina faida na hasara.Baada ya kusema haya ninakutaarifu mtoa mada na uma mzima unaoshiriki uzi huu kuwa kandambili(flip-flops) huweza kuvaliwa zaidi ya bafuni. Hata hivyo, wataalamu wa styles wameshauri wapi unaweza kuvaa na wapi hapana.Pia, unapozivaa ni mavazi gani huendana nayo.
Ndala zaweza valiwa kwenye mitoko nje ya ofisi(ile isiyo rasmi), mfano kukutana na rafiki zako pale mkitazama mpira mwisho wa wiki, ufukweni n.k
Wanashauri usivae ndala ofisini(ofisi nyingi haziruhusu,japo usishangae wengine wakaruhusu, rejea suala mtazamo hapo juu), pia usivae ndala kwenye mikutano hasa iliyo rasmi , sherehe rasmi n.k
Kuhusu kuvaa na nini, inapendekezwa(hasa kwa wanaume) ndala zivaliwe kwa suruali ya jeans ama kaptula.
Hivyo, kikubwa hapa ni kujua kuwa uvaaji hutawaliwa na mitazamo, fasheni na utamaduni. Wewe umefunzwa hivi, mimi nimefunzwa vile, wewe unapenda hiki,mimi ninapenda kile, fasheni inataka hivi, wewe unasema hapana, nitabaki hivi.Pande zote,hakuna atakaekufa kwa kusimamia anachoamini hapo. Hiyo ni tofauti na sumu ya panya,ambayo ukiibugia kiasi cha kukuondoa jibu ni moja tu, ukipona basi watu tutajiuliza na kutafuta sababu iwe ya kiroho ama maabara ya kisayansi.Ili kujifunza zaidi kuhusu uvaaaji ndala rejea kiunganishi hiki hapa chini:
Are You Breaking the Rules of Flip-Flop Etiquette? Find out Here.
Ninawasilisha