Kwa umri huo wa miezi mitatu mtoto anategemewa kuwa na uzito kati kilo 5 mpaka kilo 7.9. Hata hivyo kuna utofauti ambao hutokea kulingana na jinsia, uzito wa kuzaliwa na kasi ya ukuaji wa mtoto.
Ni muhimu ukampeleka kwa daktari ili apimwe huo uzito na kuweza kulinganishwa na urefu wake, umri wake na jinsia yake ili kuona kama vinaendana kwa uwiano unaotakiwa.
Kila la kheri.