ni sahihi kwa mwanaume.....

Nailyne

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2010
Posts
350
Reaction score
113
hivi katika maisha ya sasa ambapo unakuta mwanaume ameoa mke mwenye kipato eg. mhasibu, mhandisi, au ambaye ana shughuli zake binafsi za kumwingizia pesa ya kutosha kwa wao kama mke na mume kushare majukumu ya kuendesha familia mfano watu siku hizi wanashare ujenzi,rent,bill za nyumbani,ada za watoto et.., je ni sahihi kwa manaumwe kumpa mkewe pesa za matumizi yake binafsi? pesa kwa ajili ya mke kununua mavazi,kwenda saluni nk nk! au hii kwa sasa dhana iliyopitwa na wakati na ya kiutamaduni zaidi?? au kwa kuwa mke anauwezo wa kupata kipato haina sababu kwa mwanaume kumpa mkewe fedha za matumizi?

kwenu wadadavuzi naomba kuwasilisha!
 
hili swali zuri ngoja wadau waje wachangie tusikia am curious to know mitazamo ya watu humu......
 

Hapo umenichanganya kidogo. Au sioni vizuri dear??
 
Nailyine unakuwa kama huwajui wanawake bana? dem wa kiswahili chake ni chake hata kama ana mamilioni na cha mme/bwana/hawara ni chenu wote hata kama ni ndururu!
 
ndiyo ni haki yake kabisa kumuhudumia vitu kama mavazi salon na mengine pia kazi yake isyo sababu ya ww kutokumuhudumia huyo ni mkeo ni jukumu lako kumtunza,umeuliza swali zuri sana hope litachangiwa vilivyo mana mnajisahau sana mnapokutana na mwanamke mwenye kazi sometime hata hayo ya msingi hamyafanyi unamuachia kila kitu.
 
Nna hamu ya kusikia majibu ya hili swali...yamenikuta hayo!!
 
yani NI SAHIHI KABISA KABISA....hata kama nna kipato ...NKIOMBA NAULI NIPE,HELEA YA NGUO NIPE...WANAUME WAMEUMBWA MATESO.....nafikiri ni sahihi wtaoe na mi napewaga..japo mtu analalamika lakini ndo hivyo si wanawake tunamabo mengi wao hilo tuu aaaha.....YANI ATOE KWA MOYO 1....HATA KAMA NIMEMZIDI MSHAHARA....and i love this part.......anavyolalamika pale....lol...:wink2:
 
si sahihi angekuwa ni mamawa nyumbani hapo sawa lazima umpe mkeo hela za matumiz binafsi lakin so long as nae anafanya kaz nae mwisho wa mwezi anapokea mshahara sion tija ya kumpa hela tena,,,,,vinginevyo ni matumiz mabaya ya pesa,na mwanaume wa aina hii ni yule aliyezoea kuhonga wanawake:blah:
 
huwezi kuliziba jua na ungo!
 

Ntakupa ila siku nikijua za kwako unapeleka kwa serengeti boi........
 
Ntakupa ila siku nikijua za kwako unapeleka kwa serengeti boi........

Acha hizo bana mbona huwa hunipi mie ndo nakupa za kwangu za kwenda kula kitimoto na bia aahhh samahani nimetoa siri
 
nafikiri tabia nyingine ziachwe....hiyo iliwafaa zaidi wamama wa nyumbani...sasa mtu una kipato kizuri hata saloon upewe? na ada ya mtoto si ndo kabisa na bill za nyumba atalipa mume? tushirikiane kipato kwa maslahi ya familia na lile unaloweza afford mwenyewe we tumia hela yako....kama ni kukuonyesha moyo wake ulivyo atakuonyesha tu kwa kukupa au kukununulia vitu mara kwa mara au kukupeleka sehemu utakayofurahia.....kupewa nauli na vinginevyo its not a guarantee kuwa unatunzwa.....ila nahisi ndani wanaume wenye wanawake wenye hela lakini matumizi hayaeleweki waga wana hofu wakiondoka wao hapa duniani kama wanawake wao wataweza mudu familia.....duh!!
 

well said,,,lkn kuhudumiana ni vema pia
 


Hiyo red ndo mambo yote wanawake pia tuache kujiendekeza na kujibweteka
 
Hiyo red ndo mambo yote wanawake pia tuache kujiendekeza na kujibweteka

kwa kweli.....vitu vingine ndo maana wanaume wakienda nje...ukimuuliza anasema we shida yako nini??kwenda kwangu nje kuna ulichokosa,hela si unapata,kodi unalipa wewe.gari umenunua wewe......kama huwezi waweza enda......heeeeeee.....uomba omba mwingine siyo......:decision::decision:
 
Wanawake hua hawajibweteki, ila wanaume niwajibu wao kuwatunza wake zao. Tena wanawake tunahaki ya kuhudumi japo hua tunajihudumia wenyewe, coz siwezi toka job nataka kupita saluni kuosha nywele nimtafute jamaa yangu anipe pesa no, wengi wao huwa wanajihudumia japo ni haki yako kutunzwa. Atabaki kuona wawenzie wanapendeza wakati ye ana subiri mtu atoke huko mkuranga amtunzie mkewe.
 
Mwanamke aliyeolewa anahitaji security toka kwa mumewe. Upendo wa mume kwa mke ni moja ya vitu ambavyoonyesha mwnamke yuko salama kwa mumewe. Kumpa pesa za vitu kama saloon ni muhimu sana kwani huonyesha upendo wa mume kwa mke. Mwanamke ni mwanamke tu! haijarishi anapesa kiasi gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…