Entare nshaija
Member
- Sep 30, 2016
- 28
- 18
Kama mada ilivyo hapo juu.
Shule ya msingi Goziba ni shule ya kisiwani Goziba kilichopo katika ziwa Viktoria wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera iliyoanzishwa tangu mwaka 2003.
Mtendaji wa kata ya Goziba ndugu Magreth Peter Mashenji aliunda kikosi kazi ili kiweke mipaka kwenye shule ya msingi Goziba. Kikosi hicho kiliundwa mwezi December mwaka 2022 kipindi cha likizo kikihusisha baadhi ya wenyeviti wa vitongoji vya kata hiyona mwenyekiti wa kijiji Goziba na kikaweka mipaka 6/1/2023 zikiwa zimebaki siku 2 kufungua shule.
Mipaka hiyo iliwekwa wakiwa na madai ya kukosoa mipaka iliyokuwepo tangu shule inaanzishwa ila cha ajabu mtendaji hakumshirikisha mwalimu mkuu wa shule hiyo, hakumshirikisha mwenyekiti wa kamati ya shule, wala majirani wa shule hiyo.
Mwalimu mkuu alipofika shuleni siku ya kufungua shule 9/1/2023 akagundua uwepo wa mipaka hiyo ikabidi ampigie simu mwenyekiti wa kijiji kumuuliza kama ana taarifa za hiyo mipaka, mwenyekiti alikana kuwa hakuwa taarifa za hiyo mipaka (japo baadhi ya majirani wa shule walimuona akishiriki zoezi hilo la kuweka mipaka.)
Mwalimu mkuu alihamua kuweka kikao cha dharura na walimu wenzake pamoja na mwenyekiti wa kamati ya shule ili wajadili jambo kwa pamoja. Wakatoka na hitimisho kuwa wanakwenda kuiondoa mipaka hiyo kwa sababu hata mwenyekiti wa kijiji hicho alibisha kuwa hakuwa taarifa za mipaka hiyo hivyo ikachukuliwa kuwa iliwekwa na wahuni.
Baada ya kuing'oa mipaka hiyo taarifa zikamfikia mtendaji wa kata, akamuita mwalimu mkuu ofisini kwake. Mwalimu mkuu alipofika ofisini alimkuta mtendaji amefura na kuwaita walimu wapumbafu huku akiwatishia kuwaweka ndani.
Hapohapo kikafanyika kikao cha dharura kwenye kata na miongoni mwa wajumbe ni pamoja na mwenyekiti aliyepigiwa simu akasema hakuwa na taarifa za mipaka. Walimu waliomba kushiriki kikao hicho ila akakubaliwa mwl mkuu tu. Hitimisho la kikao hicho likatoka kuwa mtendaji habadili maamuzi na kumuhamuru mwl mkuu arudishe mipaka hiyo.
Swali ni
1: Je, mtendaji wa kata anaweza kuhamua muda wowote kupunguza au kuongeza eneo la shule?
2: Kama lengo lilikuwa zuri la kupunguza eneo la shule kwa nini vikao vya kupunguza eneo la shule asishirikishwe mwl mkuu?
3: Kwanini walivizia vikao hivyo viwekwe na mipaka vifanyike kipindi cha likizo?,
4: Kama mipaka ilikuwa na lengo jema, kwanini hata mwenyekiti wa kijiji alipopigiwa simu akakana taarifa za kuwa na taarifa za hiyo mipaka?
Mwisho naomba mamlaka zinazohusika zimulike suala hili kwa kina ili kujua lengo la mtendaji huyu kutenga eneo hili la shule kinyemela.