Ni sahihi uongozi wa kata kuweka mipaka kwenye shule iliyojengwa kipindi kirefu bila mwalimu yeyote au jirani kuwepo ili kuonesha mipaka?

Ni sahihi uongozi wa kata kuweka mipaka kwenye shule iliyojengwa kipindi kirefu bila mwalimu yeyote au jirani kuwepo ili kuonesha mipaka?

Joined
Sep 30, 2016
Posts
28
Reaction score
18
Kama mada ilivyo hapo juu.

Shule ya msingi Goziba ni shule ya kisiwani Goziba kilichopo katika ziwa Viktoria wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera iliyoanzishwa tangu mwaka 2003.

Mtendaji wa kata ya Goziba ndugu Magreth Peter Mashenji aliunda kikosi kazi ili kiweke mipaka kwenye shule ya msingi Goziba. Kikosi hicho kiliundwa mwezi December mwaka 2022 kipindi cha likizo kikihusisha baadhi ya wenyeviti wa vitongoji vya kata hiyona mwenyekiti wa kijiji Goziba na kikaweka mipaka 6/1/2023 zikiwa zimebaki siku 2 kufungua shule.

Mipaka hiyo iliwekwa wakiwa na madai ya kukosoa mipaka iliyokuwepo tangu shule inaanzishwa ila cha ajabu mtendaji hakumshirikisha mwalimu mkuu wa shule hiyo, hakumshirikisha mwenyekiti wa kamati ya shule, wala majirani wa shule hiyo.

Mwalimu mkuu alipofika shuleni siku ya kufungua shule 9/1/2023 akagundua uwepo wa mipaka hiyo ikabidi ampigie simu mwenyekiti wa kijiji kumuuliza kama ana taarifa za hiyo mipaka, mwenyekiti alikana kuwa hakuwa taarifa za hiyo mipaka (japo baadhi ya majirani wa shule walimuona akishiriki zoezi hilo la kuweka mipaka.)

Mwalimu mkuu alihamua kuweka kikao cha dharura na walimu wenzake pamoja na mwenyekiti wa kamati ya shule ili wajadili jambo kwa pamoja. Wakatoka na hitimisho kuwa wanakwenda kuiondoa mipaka hiyo kwa sababu hata mwenyekiti wa kijiji hicho alibisha kuwa hakuwa taarifa za mipaka hiyo hivyo ikachukuliwa kuwa iliwekwa na wahuni.

Baada ya kuing'oa mipaka hiyo taarifa zikamfikia mtendaji wa kata, akamuita mwalimu mkuu ofisini kwake. Mwalimu mkuu alipofika ofisini alimkuta mtendaji amefura na kuwaita walimu wapumbafu huku akiwatishia kuwaweka ndani.

Hapohapo kikafanyika kikao cha dharura kwenye kata na miongoni mwa wajumbe ni pamoja na mwenyekiti aliyepigiwa simu akasema hakuwa na taarifa za mipaka. Walimu waliomba kushiriki kikao hicho ila akakubaliwa mwl mkuu tu. Hitimisho la kikao hicho likatoka kuwa mtendaji habadili maamuzi na kumuhamuru mwl mkuu arudishe mipaka hiyo.

Swali ni
1: Je, mtendaji wa kata anaweza kuhamua muda wowote kupunguza au kuongeza eneo la shule?

2: Kama lengo lilikuwa zuri la kupunguza eneo la shule kwa nini vikao vya kupunguza eneo la shule asishirikishwe mwl mkuu?

3: Kwanini walivizia vikao hivyo viwekwe na mipaka vifanyike kipindi cha likizo?,

4: Kama mipaka ilikuwa na lengo jema, kwanini hata mwenyekiti wa kijiji alipopigiwa simu akakana taarifa za kuwa na taarifa za hiyo mipaka?

Mwisho naomba mamlaka zinazohusika zimulike suala hili kwa kina ili kujua lengo la mtendaji huyu kutenga eneo hili la shule kinyemela.
 
Babati mbaya hapa JF hakuna walimu Wala maafisa watendaji,watu wote humu JF Ni wafanyabiashara na walioajiriwa wanafanya kazi UN.

Pole mkuu.
 
hana mamlaka hayo! kama kafanya hivyo bila kushirikisha majirani wa eneo hilo, nenda kayangoe, then suluhu itaanzia hapo!
Yameshangolewa na ndo jambo lililompelekea mtendaji huyo kutukana na kumuhamuru mwl mkuu kuirudisha hiyo mipaka
 
Kwahiyo amepunguza eneo la shule? Je, eneo ambalo limepunguzwa limepewa nani? Isije kuwa labda wanataka kujenga shule nyingine halafu nyie kwa vile mnalima hapo mnang'ang'ania.
 
Kwahiyo amepunguza eneo la shule? Je, eneo ambalo limepunguzwa limepewa nani? Isije kuwa labda wanataka kujenga shule nyingine halafu nyie kwa vile mnalima hapo mnang'ang'ania.
Elewa msingi wa mada, ni sahihi mtendaji kupunguza eneo la shule bila kushirikisha uongozi wa shule? Mambo ya kujenga shule nyingine au matumizi mengine yangejulikana endapo kungekuwa na vikao vya uwazi ambapo mwl mkuu pia angekuwa mjumbe wa kikao hicho. Sio udakie tu. Kumbuka mwl mkuu ni msimamizi mkuu wa maeneo ya shule.
 
Eneo la shule lipo chini ya kijiji, kama Kijiji kimeamua kutenga eneo lao kwa ajili ya matumizi mengine wewe ni nani hadi uwazuie? Wewe endelea na kazi yako ya kufundisha hayo mengine aachana nayo, mtendaji wa kata ni mkubwa kwako kama amefanya hivyo basi anayo sababu ya kutosha kufanya hivyo.
 
Elewa msingi wa mada, ni sahihi mtendaji kupunguza eneo la shule bila kushirikisha uongozi wa shule? Mambo ya kujenga shule nyingine au matumizi mengine yangejulikana endapo kungekuwa na vikao vya uwazi ambapo mwl mkuu pia angekuwa mjumbe wa kikao hicho. Sio udakie tu. Kumbuka mwl mkuu ni msimamizi mkuu wa maeneo ya shule.
Wahaya ni watu wa hovyo sana sasa wewe hilo linakuathiri nini?

Mnaacha kulilia ukali wa maisha upungue mnalilia mipaka ya ardhi ya serikali?
 
Mtoa mada embu fafanua zaidi, why mtendaji kata awe na uwezo wa kupima mipaka?mipaka sio kazi ya mwalimu au mtendaji ,wapi idara ya Ardhi na ramani ya wilaya, hawa ndio wataalamu wa kufanya hii kazi...au ndio yale yale ya shithole country, kila mmoja anajifanyia anavyotaka?,unanikimbusha wakati nipo mwanafunzi pale kinondoni primary school, ugomvi wa mama siri yako (aliyekua anamiliki zile buses za siri yako)na uongozi wa shule!,end of the day shule ilijikuta inapoteza more than 40%ya ardhi yake iliyokua haijaendelezwa!nchi hii ina vituko vingi sana
 
December 2023 Mara January 06 2023 yaani tumetoka mbele tunarudi nyuma? Na kama wewe ni Mwl kwa uandishi huu kazi ipo.
 
Back
Top Bottom