Ni sahihi wateja kuuziwa vifungashio baada ya kununua bidhaa tena za pesa kubwa tu?

Ni sahihi wateja kuuziwa vifungashio baada ya kununua bidhaa tena za pesa kubwa tu?

Nilishawahi ghairisha kununua mchele wa 25kgs baada ya muuzaj kuniuliza aniwekee wapi. Nilimuuliza kivipi, akadai hana mfuko, aidha nilipie 1000 kwa ajili ya kiroba.

Nilimwambia abaki na mchele wake tu.
Ila wafanyabiashara bongo wana kiburi sana, sehemu nyingi tu huwa naona mfanyabiashara hauzi bidhaa au kutoa huduma kwa sababu hana chenji!
 
Muuzaji anapaswa kuweka bajeti ya vifungashio kwa wateja wake.

Kwani yeye anapoenda kununua iwe viwandani ama kwenye maduka makubwa ya jumla?

Kuna bidhaa zinakuwa na vifungashio tayari, na bado unauziwa.

Ule ni uhuni kumtoza mnunuzi gharama ya kubebea bidhaa alivyonunua dukani kwako. Hii tabia ipo hasa kwenye suppermarket.

Binafsi, ukinitoza kibebeo, napunguza bidhaa nachua nazo weza kubeba ama sehem wanaponipa kibebeo.
Ukipunguza bidhaa haumpunguzii kitu mfanyabiashara, mda tu vitanunuliwa

Kuhusu mwenye duka/mfanyabiashara kuuziwa bidhaa zikiwa na vifungashio ni teari wanaomuuzia wameshapiga mpaka hesabu ya kifungashio so pesa ya kifungashio imepigiwa mahesabu.
 
Hili suala la mtu kununua vitu/ bidhaa unakuta vinafika hata elfu 20,000 au zaidi halafu muuzaji anataka ulipie na kifungashio mia tano kubeba bidhaa ulizonunua kwake imekaaje?

Ni kwamba wafanyabiashara huwa wanafikiri bidhaa tunaweza kubeba mkononi bila vifungashio au vipi?!
Sio sahihi, kifungashio anatoa anaeuza bidhaa. Mf. Sukari ni lazima akuwekee kwenye mfuko.
 
Ndugu sizan kama kuna haja ya kutumia nguvu zako kudiscuss vitu vidgo km ivyo najua inakuboa sio ww tu ata sisi kinatukera sana ila sasa utafanyaje?

Na hii tabia iko sana masokoni unaenda sokon una fanya maemezi ata ya 100k tena kwa mtu mmoja ukimaliza muuzaji anakuuliza una mfuko unabaki tu kushangaa inabidi utoe pesa ingne ununue mfuko au gunia,

Sasa utafanyaje utabishana nao kila sku utagombana nao kila sku sana sana ni sku ingne ukienda sokon beba mfuko wako au gunia basi.
 
Ndugu sizan kama kuna haja ya kutumia nguvu zako kudiscuss vitu vidgo km ivyo najua inakuboa sio ww tu ata sisi kinatukera sana ila sasa utafanyaje?

Na hii tabia iko sana masokoni unaenda sokon una fanya maemezi ata ya 100k tena kwa mtu mmoja ukimaliza muuzaji anakuuliza una mfuko unabaki tu kushangaa inabidi utoe pesa ingne ununue mfuko au gunia,

Sasa utafanyaje utabishana nao kila sku utagombana nao kila sku sana sana ni sku ingne ukienda sokon beba mfuko wako au gunia basi.
Cha kufanya ukienda kununua bidhaa kama mtu akupi kifungashio muachie bidhaa zake.
 
Hayo mambo nimeyakuta yanafanyika huko Dar, huku kwetu hatununui vifungashio/mifuko
tena kuna maduka wana mifuko ya kila size. quality nzuri na ipo printed na brand zao ila hatununui. Labda sokoni changanyikeni tunakonunua bidhaa za jikoni na mboga ndio either uende na mfuko wako au ununue toka kwa vijana wanatembea tembea kuuza mifuko
 
Mi juzi kati hapa niliumia sana, nilienda kwenye mgahawa kununua chakula cha 3000, baada ya kufungiwa nikatoa 5000...nashangaa narudishiwa 1500...kuhoji, akasema jero ni ya kifungashio. Kidogo nirudishe chakula kwa sababu ile buku2 iliyotakiwa kubaki ilikuwa na kazi nyingine.
Ilipaswa akuambie mapema
 
Huu ujinga ata Malls kubwa upo. Tena ukinunua sabuni, vyakula, wanatenganisha vifungashio viwili. Na ikibaki chenji 200 wanakupa pipi. WTF???
 
Hili siyo sawa kabisa hasa kwa Shoppers Plaza wana mchezo huo miaka mingi sana. Unachagua bidhaa zako kwa mujibu wa hela uliyonayo. Then ukifika kwa cash counter anaweka bidhaa kwenye mfuko ulioandikwa Shoppers Plaza.

Surprisingly anakuchaji na huo mfuko ambao ukishabeba tu unaanza kuwatangazia maduka yao ya Shoppers Plaza bila malipo.

Naamini tukilalamika kwa FCC wanaweza kuchukua hatua
Mkuu Stuxnet hapo kwenye kuwatangazia kiukweli sio sawa hata kidogo ila kwenye kununua mfuko naona ni sawa kwa sababu gharama za mfuko ziko nje ya gharama za bidhaa. Kwa mfanyabiashara makini kama mimi huwa nikiweka bei naweka na gharama za mifuko kabisa ili kuondoa usumbufu kwa mteja. Hii mifuko ambayo sio plastic ni bei ghali.
 
ikiwa umetumia matumizi ya gharama kubwa basi hapo ni vizuri akupe mfuko, ila kwa ishu za buku jero sijui buku mbili mia tano hapo ni kuwaonea tu.
 
Back
Top Bottom