Ni sahihi wateja kuuziwa vifungashio baada ya kununua bidhaa tena za pesa kubwa tu?

Nilishawahi ghairisha kununua mchele wa 25kgs baada ya muuzaj kuniuliza aniwekee wapi. Nilimuuliza kivipi, akadai hana mfuko, aidha nilipie 1000 kwa ajili ya kiroba.

Nilimwambia abaki na mchele wake tu.
Ila wafanyabiashara bongo wana kiburi sana, sehemu nyingi tu huwa naona mfanyabiashara hauzi bidhaa au kutoa huduma kwa sababu hana chenji!
 
Ukipunguza bidhaa haumpunguzii kitu mfanyabiashara, mda tu vitanunuliwa

Kuhusu mwenye duka/mfanyabiashara kuuziwa bidhaa zikiwa na vifungashio ni teari wanaomuuzia wameshapiga mpaka hesabu ya kifungashio so pesa ya kifungashio imepigiwa mahesabu.
 
Sio sahihi, kifungashio anatoa anaeuza bidhaa. Mf. Sukari ni lazima akuwekee kwenye mfuko.
 
Ndugu sizan kama kuna haja ya kutumia nguvu zako kudiscuss vitu vidgo km ivyo najua inakuboa sio ww tu ata sisi kinatukera sana ila sasa utafanyaje?

Na hii tabia iko sana masokoni unaenda sokon una fanya maemezi ata ya 100k tena kwa mtu mmoja ukimaliza muuzaji anakuuliza una mfuko unabaki tu kushangaa inabidi utoe pesa ingne ununue mfuko au gunia,

Sasa utafanyaje utabishana nao kila sku utagombana nao kila sku sana sana ni sku ingne ukienda sokon beba mfuko wako au gunia basi.
 
Cha kufanya ukienda kununua bidhaa kama mtu akupi kifungashio muachie bidhaa zake.
 
Hayo mambo nimeyakuta yanafanyika huko Dar, huku kwetu hatununui vifungashio/mifuko
tena kuna maduka wana mifuko ya kila size. quality nzuri na ipo printed na brand zao ila hatununui. Labda sokoni changanyikeni tunakonunua bidhaa za jikoni na mboga ndio either uende na mfuko wako au ununue toka kwa vijana wanatembea tembea kuuza mifuko
 
Ilipaswa akuambie mapema
 
Huu ujinga ata Malls kubwa upo. Tena ukinunua sabuni, vyakula, wanatenganisha vifungashio viwili. Na ikibaki chenji 200 wanakupa pipi. WTF???
 
Mkuu Stuxnet hapo kwenye kuwatangazia kiukweli sio sawa hata kidogo ila kwenye kununua mfuko naona ni sawa kwa sababu gharama za mfuko ziko nje ya gharama za bidhaa. Kwa mfanyabiashara makini kama mimi huwa nikiweka bei naweka na gharama za mifuko kabisa ili kuondoa usumbufu kwa mteja. Hii mifuko ambayo sio plastic ni bei ghali.
 
ikiwa umetumia matumizi ya gharama kubwa basi hapo ni vizuri akupe mfuko, ila kwa ishu za buku jero sijui buku mbili mia tano hapo ni kuwaonea tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…