kama mtanzania napenda kumuona mtanzania mwenzangu akiipeperusha vyema bendera yetu, nani ambaye hapendi kumuona samatta akichezea epl, bundesliga, la liga, league 1 ama serie A ? Hakika tunapenda sana kumuona lakini kwa mwelekeo wa samatta hatafika huko, hapo alipo ndio kafika na asipokuwa makini Genk inaweza kumuacha akajikuta anaporomokea timu ya chini zaidi, akaishia kwenda sweeden, south africa, agypt, morroco na kwingineko.... kwa nini nasema haya ?
1. umri unamtupa, namkadiria ana 27-30, japo passport yake inasoma 24. kwa huu umri alio nao sasa anatakiwa ndio afikie peak kwenye kiwango chake lakini ni wa kawaida sana, bahati nzuri tangia msimu uliopita anapata namba pale Genk lakini kiwango chake (ufungaji magoli) sio mzuri. sina takwimu sahihi lakini sidhani kama amefunga goli 50 tangia atue kule, japo msimu wa kwanza hakuwa anapata muda mwingi wa kucheza, lakini tangia msimu uliopita anapata namba, hana cha kusingizia tena.
2. nafasi anayocheza(striker) inamgharimu sana, angekuwa midfilder, winger au beki kwa jinsi anavyojituma na spirit aliyonayo pengine kwa sasa tungekuwa tunaongea mengine, hata acheze vizuri vipi, hata atoe assist nyingi bado ataonekana kawaida, anatakiwa azifumanie nyavu kwa kiwango cha juu sana.
ukweli mchungu