Ni sawa gari ya auto kushituka fulani gia inapochange..

Ni sawa gari ya auto kushituka fulani gia inapochange..

Du mafundi wako wengi kweli.Mwingine anasema hiyo ni gearbox ndiyo inasheeda.Hawa ndiyo wale unawapelekea gari gereji inatembea badaye unaenda kuiondoa kwa breakdown.maana hapo kunakuwa tayari kuna mtu amejifunzia ufundi hilo gari
 
Kama ushaendesha manual ,
ATA auto nazo huwa unazckia pale unapokanyaga mafuta na Gia zna change
Hata hizo manual kama unaendesha vizuri gear huwa hazishtuki ila unasikia badiliko la mlio wa injini pale unapobadilisha. Achunguze vizuri kama ni uendeshaji mbovu au gear box inamatatizo.
 
gear box ya gari lako ina mechanical failures, hii hutokea pale gear inapochelewa kubadilika na hatimae kubadilika gafla, jambo ambalo husababisha mshtuko. Gear za automatic transmitted vehicles zinapobadilika hazitakiwi kushtuka kma ilivo manual transmitted vehicles.
 
Gearbox hio ikachekiwe kama ina tatizo.

Gari ya automatic hata ukanyage mafuta vipi na uwe spidi gani huwezi pata mshtuko wa kubadilisha gear, yaani utajua gear imebadilika kwa kutizama rpm au kusikilizia mvumo wa mashine basi. Ukiona inashtuka mfano kama ina kusukuma iv ujue kuna shida
 
Hiyo gear box ya gari yako itakuwa na shida, ndani ya gearbox kuna vidude vinaitwa solenoids hivyo kazi yake ndiyo kuabsorb hiyo shock gear zinapobadilika ukiwa unaendesha hizi gari za automatic, sasa ukikuta vimepiga short na kimoja au viwili vimeungua ndiyo utaanza kusikia huo mshituko wakati gear zinabadilika... ningekushauri nenda kwa wale mafundi wa gearbox ambao wana zile mashine za troubleshoot, wakuchekie tatizo maana kama vina vimeungua huwa inaonyesha pale then wataifungua gear box na kubadilisha. Ukitaka kutapa service nzuri nenda Ilala pale pembeni ya machinga complex, opposite na zinakopakia gari za Mbagala muulizie fundi anaitwa "Mdudu" ni guru wa gearbox hizi za auto atarekebisha hilo tatizo na uzuri pale spare parts ni rahisi kupatikana maana maduka yapo hapo hapo.
 
Kuna kushtuka na ile kushtuka kama inasukuma.

Kama inashtuka kama inasukuma basi kuna shida hapo mkuu
 
Back
Top Bottom