Hiyo gear box ya gari yako itakuwa na shida, ndani ya gearbox kuna vidude vinaitwa solenoids hivyo kazi yake ndiyo kuabsorb hiyo shock gear zinapobadilika ukiwa unaendesha hizi gari za automatic, sasa ukikuta vimepiga short na kimoja au viwili vimeungua ndiyo utaanza kusikia huo mshituko wakati gear zinabadilika... ningekushauri nenda kwa wale mafundi wa gearbox ambao wana zile mashine za troubleshoot, wakuchekie tatizo maana kama vina vimeungua huwa inaonyesha pale then wataifungua gear box na kubadilisha. Ukitaka kutapa service nzuri nenda Ilala pale pembeni ya machinga complex, opposite na zinakopakia gari za Mbagala muulizie fundi anaitwa "Mdudu" ni guru wa gearbox hizi za auto atarekebisha hilo tatizo na uzuri pale spare parts ni rahisi kupatikana maana maduka yapo hapo hapo.