Ni sawa tunapata mshiko wa Mama kanisani kwetu, lakini washirika wetu wanasemaje

Ni sawa tunapata mshiko wa Mama kanisani kwetu, lakini washirika wetu wanasemaje

NewPage

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
1,380
Reaction score
2,236
Baada ya Harambee ya Dr, Mwigulu Nchemba kanisani kwa WaLutheri Singida Jumapili ya juzi tarehe 29 Juni, 2025, mama akichangia TZS 50,000,000/- kati ya zaidi ya TZS one billion iliyopatikana, waumini wengi waliloloma wakionesha Kanisa la KKKT ni kibaraka wa Serikali hii.

Wengi wanajisikia vibaya kwa KKKT kujitenga na misimamo ya WaKatoliki, ukizingatia Malasusa mwenyewe alichagiza kuwepo kwenye Harambee hiyo!

Washirika wengi wa KKKT wanajisikia aibu kwa misimamo ya juu kabisa ya KKKT, hasa kutokana na kiburi cha uongozi wa juu kuziba masikio kuhusu mambo ya ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwepo kupoteza na kuua wananzengo!
 
Back
Top Bottom