Mabadiliko ya sheria za Hifadhi ya Jamii (Social Security Laws Amendment), 2012 yaliondoa kipengele cha uwepo wa fao la kujitoa kwenye sheria ya kila mfuko (maana kila mfuko wa pensheni unayo sheria yake inayotaja mafao yanayotolewa na mfuko husika).
Hivo bas, wabunge walipitisha mabadiliko yale na hivyo automatically vipengele vilivyokua vinataja FAO LA KUJITOA (withdraw) viliondolewa.
Nasikitika kusema kwamba inawezekana kabisa kwamba mabadiliko yalipitishwa bila kujua haswa ni KITU KIPI HASA KINABADILISHWA na matokeo yake wakajikuta wame -repeal vifungu vilivyokua vinasema " mafao yanayotolewa na mfuko chini ya sheria hii ni......(FUTA -Withdraw)
Haikutungwa sheria kama sheria ya kusema FAO LA KUJITOA LISITOLEWE...bali kwa mabadiliko yale kurekebisha vipengele vya mafao na kutokutaja fao la kujitoa (withdraw) automatically mfuko hauwezi kulipa kwakua mfuko unalipa mafao YALIYOTAJWA TU na kila fao limewekewa utaratibu namna linavotolewa.
Sheria za mifuko yote pamoja na hao wasimamizi wa SSRA zilirekebishwa mwaka 2012 na copy ya sheria ambazo ziko embeded zinataja sheria kua ni [R.E 2015] ~maana yake ni kwamba shwria husika ni TOLEO LA 2015 (ambalo ndilo linayo hayo marekebisho ya 2012.
ONA VIELELEZO
1. Kitabu cha sheria za Hifadhi ya Jamii Toleo 2015.
2. Sheria za mifuko mmojammoja zinajieleza (hii ni NSSF)
3. Mafao ya NSSF (angalia kwa hautaona WITHDRAWAL ikitajwa, iliondolewa)
Naenda Zim.