Ni siku ya 17 leo Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la GCTC hajaonekana? Wewe unafikiri yuko wapi? Nitakupa Jibu hapa hapa 👇

Ni siku ya 17 leo Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la GCTC hajaonekana? Wewe unafikiri yuko wapi? Nitakupa Jibu hapa hapa 👇

Asije akawa ametumbukia shimoni (kuzimu) kuchukua nguvu manake kuna wachungaji wengi sana wanakwenda huko kwa bwaba wao.
Kavunja maagano na kuzimu na kukiuka masharti ya kuzimu na freemason ndio maana ghafla bin vuu kanisa linakufa

Waumini watafute makanisa mengine ya kusali
 
Kwenye huu ujinga msiwe mnamhusisha Mungu wala kujificha kwenye kivuli cha Mungu , ndo mana mambo huwa yanawaendea kombo Zaid Kwa kujidanganya kuwa mkitaja neno Munu basi mtu atawaonea huruma
Sasa ndugu, tusipomhusisha Mungu tumhusishe nani? Jezebel shetani....?

Mungu anawapenda hata vichaa na wajinga. Wote anawaita waje kwake....

Kwa hiyo, hebu tuache tumhusishe Mungu na Baba yetu hata ktk ujinga wetu....

Wewe na werevu wako, wahusishe wachawi na waganga na mashetani...
 
Gwaji ana amani ila watesi wake wanahaha usiku na mchana kwa hofu.

Sauti ya Bwana wa Majeshi ikasema " Usiogope maana mimi nipo pamoja nawe, nimekutuma wewe waambie watawala mambo haya"

Watawala sasa....hiii
Amina....🙏🏻🙏🏻
 
Mkuu The Palm Beach Salam kwako.
Shalom Shalom. Sijapendezwa na Post yako kwani baadhi ya taarifa ni misleading (Yesu alifunga kula) na zaidi ya hapo inaonekana unajaribu kumwinua mwanadamu (Gwajima) na sio Mungu. Hivi unaweza elezea ni roho ya aina gani iliyokuwa inamsukuma Gwajima kushambulia Mamlaka kwa kutumia madhabahu ya Kanisa lake? Ushauri jaribu kumtafuta Mungu kama mtu binafsi bila kumwangalia mwanadamu yeyote.
Samahani kama nimekukwaza.
Ahsante
​
Lini Gwajima alishambulia mamlaka?
Kutaja jina ni kumshambulia mtu?
 
Asije akawa ametumbukia shimoni (kuzimu) kuchukua nguvu manake kuna wachungaji wengi sana wanakwenda huko kwa bwaba wao.
Mungu Baba wa mbinguni akusamehe. Sio kosa lako....

Ni kwa sababu tu ya kukosa uelewa wa maandiko kukuwezesha kujua utendaji kazi wa Mungu ktk kuwalinda wenye haki, watoto wake na masihi/watumishi wake

Hata Mtume Paulo aliokolewa kwenye mikono ya watawala waovu na wamwaga damu kama hivi👇🏻

2 Wakorintho 11:32-33 TKU
".....Nilipo kuwa Dameski, gavana wa mfalme Areta alitaka kunikamata, hivyo aliweka walinzi nje ya malango ya jiji. Lakini baadhi ya rafiki wakaniweka ndani ya kikapu. Kisha wakaniteremsha chini kupitia dirisha lililokuwa kwenye ukuta wa mji. Hivyo nikamtoroka gavana...."​

Kwa uelewa wako huu, basi unaweza hata kutuambia na Mtume Paulo naye alitumbukia kuzimu🤔🤔🤔🤔.!!
 
Mungu Baba wa mbinguni akusamehe. Sio kosa lako....

Ni kwa sababu tu ya kukosa uelewa wa maandiko kukuwezesha kujua utendaji kazi wa Mungu ktk kuwalinda wenye haki, watoto wake na masihi/watumishi wake

Hata Mtume Paulo aliokolewa kwenye mikono ya watawala waovu na wamwaga damu kama hivi👇🏻

2 Wakorintho 11:32-33 TKU
".....Nilipo kuwa Dameski, gavana wa mfalme Areta alitaka kunikamata, hivyo aliweka walinzi nje ya malango ya jiji. Lakini baadhi ya rafiki wakaniweka ndani ya kikapu. Kisha wakaniteremsha chini kupitia dirisha lililokuwa kwenye ukuta wa mji. Hivyo nikamtoroka gavana....
"​

Kwa uelewa wako huu, basi unaweza hata kutuambia na Mtume Paulo naye alitumbukia kuzimu🤔🤔🤔🤔.!!
Zichunguzeni roho...Mungu mwenyewe ametupa uhuru wa kuzichunguza roho za watumishi wake hadi tujiridhishe kuwa wana Roho wa Kweli wa Mungu.
 
Mfungo wowote ambao unauanza baada ya kukosea labda uwe wa toba kuomba Mungu akusamehe makosa yako uliyokosea au kukosesha wengine hadi wanashindwa kuabudu kwenye huduma ulianzisha nk kwa kugeuka kuwa shetani wa kuua huduma au kanisa

Vinginevyo mfungo ni batili sijui wa kulaani maadui ubatili mtupu hata mtu afunge siku 100 au elfu moja wakati yeye ndie kasababisha kanisa kufungwa

Yona meli ilipotaka kuzama alikiri makosa mbele ya Mungu kuwa enyi waumini kwenye meli nitoseni baharini mimi ndio itakuwa salama ya Meli hii kanisani meli isizame ndio sababu ya misukosu ya meli ya hili kanisa melini ni mimi Gwajima nyie waumini hamhusiki.

Gwajima aache ujinga hata afunge siku milioni upotezaji muda akubali kuwajibika mbele za Mungu sio Mwanadamu kwa makosa kafanya

Na aache kabisa huduma kama Yona
Mungu atasema naye mbele huko ya safari
Asiachie waumini tu waamue kama kwenye meli

Yona alipoongea kuwa yeye ndie sababu .Mungu alimtoa huduma alikuwepo akampeleka Ninawi huko Akaanze upya huko huduma sio aliyokuwa nayo
1. Kosa la Gwajima ni lipi specific? Eleza kama unaweza...

2. Ibada ya mfungo ilitangazwa tarehe 1/6/2025...

3. Mfungo ukaanza tarehe 2/6/2025 siku ya J'3...

4. Uvamizi wa kanisa ukafanyika tarehe 2/6/2025 saa 5 kuelekea saa 6 usiku. Haina shaka yoyote kuwa, wachawi na waganga wapiga puri (ramli) waliona hatari ya maombi yale na kutuma mawakala wake kuja kujaribu kuyavuruga kwa kuzuia na kulifunga jengo la kukutania washirika kuomba. Shetani hana akili siku zote, hajui siri za Mungu siku zote. Yeye alifikiri kwa kuzuia jengo, Mungu hataabudiwa, maombi hayataendelea. Hajui kuwa maombi ni mawasiliano ya kiroho ktk ulimwengu wa roho. Kwamba unaweza kuwa DSM nami huku Shinyanga kwetu tukawa tunaomba kwa pamoja na interconnection ya ulimwengu wa roho ikafanyika na ngome za adui zikaanguka. Hivyo ndivyo ilivyo hata sasa. Mungu hajalala, yupo kazini...

5. Theme ya maombi ilikuwa very clear kuwa ni:
➡Kuombea taifa ili roho ya shetani ya utekaji na mauaji ikomeshwe
➡Kuombea viongozi wa vyama vya siasa wote (akiwemo mwenyekiti wako wa CCM Bi Samia Suluhu Hassan)
➡Kuombea viongozi wa serikali ili Mungu awape hekima na busara ktk maamuzi yao
➡Specific kumwombea Mwenyekiti wa CHADEMA Ndugu Tundu Lissu aliye gerezani kwa kesi ya uongo ili Mungu aweze kumrehemu na kumtoa

##Nadhani hili la Tundu Lissu ndilo lilowaudhi na kuamua kufanya uhuni walioufanya

6. Hakuna dhambi wala kosa alilofanya Mch Gwajima. Ni uonevu na utesi wa Ibilisi tu na hata hivyo hajawahi kushinda hata mara moja. Na sasa atashindwa..!
 
Zichunguzeni roho...Mungu mwenyewe ametupa uhuru wa kuzichunguza roho za watumishi wake hadi tujiridhishe kuwa wana Roho wa Kweli wa Mungu.
Mimi nimechunguza na kujiridhisha pasipo shaka kuwa, huyu ni mtumishi wa Mungu wa kweli, amebeba roho ya Kristo ndani yake..

Nawe nakushauri, don't be manipulated easily...

Mfano, nikukuuliza uniambie kosa la Askofu Gwajima hasa ni nini hata isababishe vurugu hizi, unaweza kunieleza...?
 
Mkuu The Palm Beach Salam kwako.
Shalom Shalom. Sijapendezwa na Post yako kwani baadhi ya taarifa ni misleading (Yesu alifunga kula) na zaidi ya hapo inaonekana unajaribu kumwinua mwanadamu (Gwajima) na sio Mungu. Hivi unaweza elezea ni roho ya aina gani iliyokuwa inamsukuma Gwajima kushambulia Mamlaka kwa kutumia madhabahu ya Kanisa lake? Ushauri jaribu kumtafuta Mungu kama mtu binafsi bila kumwangalia mwanadamu yeyote.
Samahani kama nimekukwaza.
Ahsante
​
Gwajima hajashambulia mamlaka, bali aliwakemea watekaji na wauaji!! Hakutaja majina ya watekaji hao wala ya wauaji hao, ila ghafla tu samia akakurupuka huko mbio! Akaanza kumshutumu na kumpa majina ya hovyo, machawa wa samia nao wakakurupuka mbio! Wanasema Gwajima anamsema "mama" wakati gwajima kasema kuhusu wanaoteka na kuua watabganyika, ila Gwajima alishatupa codes za kuwajua wauaji hao, alisema tutaanza kuwasikia wakimshambulia, na kweli haikuchukua muda mrefu tulimsikia wa kwanza akimshambulia kwa nguvu zote, baadaye mmoja mmoja wakaanza kujitokeza, Gwakima ni shujaa wetu.
 
Personally mm nilijua moto ungekuwa uleule wa enzi za Bashite. Ghafla ziiiiii, siyo poa hii. Gwajima jitokeze popote ulipo ili isije tukaamini ilikuwa ni kuyeyusha mikutano ya CDM na sakata la Lissu gerezani.
Hv haendi ht bungen? Anajificha km nguchiro?
 
Mkuu The Palm Beach Salam kwako.
Shalom Shalom. Sijapendezwa na Post yako kwani baadhi ya taarifa ni misleading (Yesu alifunga kula)
​
Unataka nikupendeze wewe?

Kama Yesu Kristo alifunga kula, kumbe mimi nimesemaje hapo?
na zaidi ya hapo inaonekana unajaribu kumwinua mwanadamu (Gwajima) na sio Mungu. ​
Kumbe mjadala unamhusu nani?

Jibu: Ni mtu, mtumishi wa Yesu Kristo aitwaye Mch Josephat Gwajima, Askofu mkuu wa makanisa ya GCTC duniani na matukio yasiyopendeza yanayoambatana naye..

Mungu hutumia shuhuda za matendo ya makuu aliyowatendea watu wengine kuwafundisha na kuwaimarisha wengine..

Nilichofanya ni narration ya kilichotokea hata Mch Gwajima kupita katikati ya polisi na wasimjue na mpaka leo hawajui aliko...!

Je, huku ni mimi kumwinua mwanadamu au Mungu mwenyewe anajiinua kupitia mtu huyu, mtumishi wake....?
Hivi unaweza elezea ni roho ya aina gani iliyokuwa inamsukuma Gwajima kushambulia Mamlaka kwa kutumia madhabahu ya Kanisa lake?​
Eleza ni kwa namna gani mamlaka imeshambuliwa hapo..

Wote tulifuatilia na kusikiliza vizuri ushauri aliotoa Mch Gwajima kwa serikali ili kutatua tatizo la utekaji, kupotea na mauaji ya watu wasio na hatia hapa nchini (specific wakosoaji wa serikali na Rais Samia) huku TISS na Jeshi la Polisi wakihusishwa matendo haya mabaya na wakati huohuo hakuna hatua zilizochukuliwa kukomesha tatizo hili...

Hapo kuna kosa gani? Na wewe unafikiri kazi ya madhabahu ya Bwana Mungu ni ipi kama sio kunena juu ya haki, kumseta shetani na uovu wake...?

Mimi nadhani wewe ndiye hujui hasa ni kitu gani unasema na kutetea...!!
Ushauri jaribu kumtafuta Mungu kama mtu binafsi bila kumwangalia mwanadamu yeyote.
Samahani kama nimekukwaza.
Ahsante
​
Here you come again...

Mchungaji wangu ni mwanadamu, mlezi wangu kiimani..

Ninayo nafasi yangu kumtafuta Mungu kibinafsi. Lakini yupo kiongozi wangu pia mchungaji ambaye Mungu kamweka pale kuwa mlezi na mshauri wangu kiroho na kiimani..

Sisi waumini tunachoshauriwa ni kupata wachungaji wema na wa kweli wa kondoo. Sio kwenda kwa wachungaji mbwa mwitu wala kondoo au wachungaji wa mshahara...

Mchungaji Gwajima ni mchungaji wangu. He's a true man of a Living God na wewe huna chochote unachoweza kunifundisha au kunishauri juu yake...!!
 
Bongo usijifanye shujaa kiherehere. Unapotea na jamii haina muda na wewe.
 
1. Jumapili ya tarehe 1/6/2025 katika Ibada ya siku ya Bwana alitangaza mfungo wa siku 7 mchana kisha jioni unafungua kwa Aidha kunywa maji au chakula chepesi kama uji nk

2. Lengo la mfungo lilikuwa kuombea taifa, kuombea viongozi wa vyama vya siasa vyote, kuiombea serikali yetu na Rais Samia na kumwombea Mwenyekiti wa CHADEMA aliyeko gerezani kwa uonevu Mh Tundu Lissu ili Mungu amrehemu na kumtoa

2. Mfungo ulianza siku ya J3 tarehe 2/6/2025. Lakini ghafla, usiku wa saa 5 siku hiyo, Polisi walivamia kanisa la makao makuu ya GCTC - Ubungo, kuvuruga kila kitu na kutaka kumkamata kiongozi mkuu wa kanisa hilo, Mch Josephat Gwajima..

3. Haikuwa mapenzi ya Mungu awe ktk mikono ya polisi wale wauaji. Katika namna ambayo haiwezi kuelezeka kwa lugha ya kawaida ya kibinadamu, alipita katikati yao, akaondoka zake na kuwaacha solemba. Toka siku hiyo, hakuna ajuaye yuko wapi...!!

MAJIBU

• Leo ni siku ya 17 tangu siku ya kuondolewa kwake na Mungu na kufichwa ambako mwanadamu asiye na kibali cha Mungu hawezi kumuona...

• Yupo, somewhere very special anaendelea na maombi ya siku aidha 21 au 40. Haya maombi ya siku 21 au 40, yeyote ayafanyaye na kumaliza, tetemeko na kishindo cha utukufu wa Mungu hushuka.

• Katika rekodi zilizopo kwenye Biblia maombi ya siku 21 au 40 kavu yalifanywa na watu kadhaa; Yesu Kristo kule nyikani, Musa ktk mlima Sinai, Eliya na Daniel nk...

• Hebu jaribu kufikiri: Hivi Mch Gwajima akitoka huko kwenye safari ya maombi ya siku 21 au pengine 40 hawa watesi wake wanaokula na kunywa kwa raha zao huku wakimkufuru Mungu watapatwa na nini..?

Ndugu, kaeni mkao wa kula. Mabaali, miungu ya Jezebel itachinjwa na kuzikwa milele siku sio nyingi. Chukua nafasi, omba na ombea watumishi wa Mungu wa kweli wote kama Mch Josephat Gwajima...

Maombi ya siku 21 (2 - 22/6/2025): Utamwona tarehe 23/6/2025 siku ya J'tatu

Maombi ya siku 40 (2/6 - 11/7/2025):
Utamwona ktk ibada kanisani tarehe 13/7/2025 J'pili

Stay cool & connected. Expect the unexpected to happen.
"...God is always good..."
​
Ninachojua mimi, yupo "safe house" mmojawapo anafundishwa uzalendo. Siku akirudi uraiani utaona tu mabadiliko.
 
Mi sijapenda, katushikashika, katupapasa, katupa uhakika.....afu kasepa, sijapenda.
Pole...

Lakini vita hii haipiganwi ktk ulimwengu wa macho ya damu na nyama...

Hivi ni vita ya kiroho, Evelyn Salt. Mikakati na mapigano yake hufanyika ktk ulimwengu mficho (Spiritual realms)..

Unafikiri ni kwanini wanamtaka ajitokeze?

Ni kwa sababu wanataka wapigane naye ktk ulimwengu physical (mahakamani na polisi na ktk mamlaka zingine za kidunia) ambao wao ndio uwanja wao wa mapambano ili wamshinde kirahisi..

Uwanja wa vita wa kiroho, shetani anauchukia vibaya kwa sbb...

By the time anatokeza, VITA ITAKUWA IMESHAPIGANWA, IMEISHA NA MUNGU KAJITWALIA USHINDI WAKE KUPITIA MTUMISHI WAKE...!

Nasi tusuache kuomba na kupigana. Na usiache kumwombea mtumishi tafadhali..
 
Back
Top Bottom