Ni Simba koko FC au Panya SC?

Ni Simba koko FC au Panya SC?

MWAKA JANA KULIKUWA NA TETESI KUWA KUNA KIONGOZI WA SIMBA ALIKAMATWA AKIPULIZIA DAWA KWENYE VYUMBA VYA WACHEZAJI WAKATI WA MAPUMZIKO. KAMA ILIKUWA NI KWELI:-
- JEE KIONGOZI HUYO NI NANI NA KWA NINI HAJATAJWA HADHARANI MPAKA LEO ILI KUKOMESHA HUJUMA KAMA
HIZO?
- JEE KIONGOZI HUYO BADO YUPO MADARAKANI NA KAMA BADO YUPO MADARAKANI JE HAWEZI KUBADILISHA STAILI
YAKE HUJUMA?
- JEE UONGOZI BAADA YA KUMGUNDUA ULICHUKUWA HATUA GANI STAHIKI?

MASWALI YOTE HAPO JUU YANAKUJA KWA SABABU UKIANGALIA SIMBA ILIKUWA KWENYE MOTO MKALI LAKINI BAADA TU YA MAPUMZIKO KUPISHA YANGA NA AZAM KUMALIZIA VIPORO VYAO SIMBA ILIKUJA KUWA UCHOCHORO WA AJABU. WACHEZAJI WAKAWA HAWANA MORALI, WANACHEZA KAMA WAMELAZIMISHWA UTAFIKIRI WAMEFUNGWA MAWE MIGUUNI.
 
........Kama ungekuwa shabiki wa wa team ya matopeni katika nyakati kama hizi ndio ungekiri kuwa aliyeanzisha SUMU hakuwa mjinga.. Kama unabisha waulize wenyewe
 
Mkuu Amavubi mimi ningeomba tukubaliane at Principle kwamba Uongozi chini ya Mwenyekiti Aveva Umefeli...na umeshindwa ku achieve hata kile kidogo ulichopanga....Na hii imetokana na maamuzi ya mtu mmoja tena maamuzi ya kibabe yasiyo na maslahi kwa timu....Leo hao wachezaji wetu tuliowatengeneza wanafukuzwa kibabe na huyo Hanspope....Mchezaji akidai stahiki zake anaundiwa zengwe na kuonekana mbaya....Lakini tatizo lipo...Huyu Pope yeye anafanya kama anakopesha klabu lakini kwa malengo ya kuja kujilipa mara kadhaa zaidi......

Udhaifu wa Simba unachagizwa na usajili mbovu usio wa kimpira unaofanywa na Pope....Mwalimu wa timu hana nafasi..Ukiniuliza leo kwa nini timu haina kocha mkuu kwa karibu nusu msimu..nadhani hata jibu na wewe hauna...

Leo hii ukiuliza malipo ya fedha za Okwi na Sammatta yako wapi huwezi kupewa jibu la kueleweka.

Katika mfumo wa sasa wa simba kuongozwa kama chama cha siasa ...hakutakuwa na mafanikio hata miaka 200 ijayo



Kwa mfano hili unalolosema hapa.....Kwa nini klabu kubwa kama simba imtegemee Pope.....Lazima sisi tukae tujitafakari...Timu yetu ina miaka takribani 90 ya uhai wake...ivi kweli hatuwezi kuifanya klabu ijitegemee?

Lakini najua njia rahisi ambayo pia imechukuliwa na TP Mazembe ni kubadili mfumo wa timu.....Kwenda kwenye kampuni....Ukiweza ku list shares watajitokeza wanunuzi wa hisa....unaweza ku issue only 50% na ku raise funds za kutosha tu.Tunachokitaka sisi washabiki na wanachama ni ushindi.....Na kwa timu yetu ilivyo...the moment itaapokuwa na guts za kifedha ...hakuna timu yoyote Afrika inaweza kutufunga

Katika mfumo wa kampuni discipline itakuwepo....wachezaji watalipwa...kocha atasajili...timu itakuwa na viwanja na assets za kutosha...Lakini Pia Simba Sports Club itaweza kuanzisha michezo mingine kama Netbol,Basket Ball,Kuogelea na kadhalika

Labda tujadiliane ugumu hasa wa kubadili mfumo ni nini?
Kwangu upo sahihi sana kuna siku penye uzi wetu wa yanga niliwahi kuandika kuhusu mafanikio haya ya hivi karibuni ya yanga nikasema jamani pamoja na haya je timu zetu hizi kongwe zinastahili kuwa hapa?timu hazina sources of income ambazo ni sustainable nikasema siku manji akikaa pembeni je hali itakuwaje?mitaji mikubwa sana hizi timu inazo nao ni wapenzi na mashabiki ukiweza hata kushawishi wapenzi kununua gazeti la yanga imara au ngurumo za simba kwa tshs 500 wapenzi wakaeleweshwa pata hata watu laki 3tanzania nzima je wanakosekana?leo mtu yupo khiari avae jezi ya united au liverpool why?viongozi wetu wana katisha tamaa timu hazieleweki bado tuna safari ndefu.
 
Back
Top Bottom