Unahisi kuna lugha ngapi duniani?
6,500-7,117.
Tena hizi ni zile zinazojulikana na zikiwa kwenye hatari ya kupungua.
Vipi kuhusu zile ambazo hazijulikani?
Wewe je unajua na kuzungumza lugha ngapi mbali na Kiswahili, Kiingereza na lugha ya kabila yako (Kilugha)?
(Washiriki wa mafunzo ya data Data4Her yaliyoandaliwa na Tanzania Data Lab)
Wakati tunaendelea kujipambanua Artificial Intelligence imefanikiwa kutumia lugha chache kati ya hizo kwa kutumia kompyuta (au vifaa vinavyofanana na hivyo) kuweza kurahisisha na kuwasilisha matakwa/mahitaji ya binadamu.
Lugha ikiwa ni mojawapo ya mafanikio makubwa ya binadamu, ndiyo maana siyo ajabu kuona artificial intelligence ikiweka nguvu kubwa sana kuihusanisha na mojawapo ya kipengele chake ambacho ni Natural Language Processing kama tuwaonavyo Alexa na Siri.
Natural Language Processing (NLP) inahusisha Natural Language Understanding (NLU) na Natural Language Generation (NLG). NLU ni kusaidia kifaa (kompyuta au kinachofanana na hicho) kusoma maandishi/sauti kwa kuiga uwezo wa binadamu kuielewa lugha husika, yaani (human to machine) NLG ni kuiga uwezo wa binadamu kutengeneza maandishi kwa lugha husika yaani (machine to human).
NLP huchambua kiasi kikubwa cha data maandishi kwa ufasaha na kung’amua maana halisi ya lugha na kutohoa taarifa muhimu au kutoa ufupisho kama kwenye madodoso, mitandao ya kijamii au taarifa kubwa.
(Picha kutoka mtandaoni; unsplash)
Kukiwa na takribani watumiaji intaneti zaidi ya milioni 50 Tanzania na zaidi ya nusu yake wakiwa wanamiliki simu tunaweza kuona namna teknolojia imedhamiria kuleta mapinduzi ya hali ya juu katika maeneo mbalimbali iwe afya, huduma za fedha (benki na mawakala), elimu, kilimo, sheria, huduma za kijamii na zingine kama biashara ambayo ndiyo lengo letu hapa kupitia matumizi ya NLP.
Kutokana na shughuli nyingi kwa sasa kufanyika mtandaoni wafanyabiashara hawana budi kuwafuata huko wateja wake, yaani kwenye majukwaa ya kimtandao ambapo kwa watumizi wa mitandao ya kijamii inakadiriwa kufikia idadi ya watu 5.40 milioni kwa Tanzania,wakigawanywa kama; twitter 56.62%, instagram 3.18%, facebook 21.23%, pinterest 11.43%, youtube 5.9%, tumblr 1.2%.
Hivyo katika mchakato wa kuwafikia / kuwafikishia huduma au bidhaa inapaswa kujua vile namna wanafikiria na kuhisi kuzihusu, kama isemavywo “ mteja ni mfalme” na “mteja hakosei” hivyo katika kundi la watu zaidi ya milioni 60 mfanyabiashara unahitaji usaidizi katika hili ndipo matumizi ya NLP huingia.
Wanasema ukitaka kumuua nyani usimuangalie usoni, katika kuwasiliana na wateja wetu kupitia maonyesho, warsha au matamasha ambapo tunakutana nao uso kwa uso kuna wakati huweza kuona sijui tuiite aibu au vipi kukwambia usoni kuhusu bidhaa au huduma yako (kasoro wale wenye ujasiri wa kufanya hivyo) hivyo basi wafanyabiashara hutumia madodoso, na vipeperushi dijitali kuwapa nafasi wateja kuelezea maoni yao.
Sasa tukiwa wakweli, fikiria kupokea mirejesho/maoni/mapendekezo/pongezi 500 kwa siku, zingine huweza hata kukupita na kuonekana kama umedharau, hutilii maanani. Hivyo kuepusha hili teknolojia inakurahisishia kazi ya kuchambua taarifa zote hizi na kukupunguzia gharama ya huenda ingekubidi umuajiri mtu aweze kufanya hii kazi.
Basi, unaweza kutumia vipengele viwili vya NLP kufikia lengo navyo ni;
Sentiments analysis hii hutumiwa zaidi kwenye madodoso wanayojaza wateja, maoni, mapendekezo na mirejesho yao kwenye majukwaa ya kimtandao hasa mitandao ya kijamii ambayo hugawanywa kwenye makundi mawili: Hasi/Chanya au zaidi kwa kadiri ya mahitaji na itakavyoonekana sahihi na kufaa.
Sentiments analysis hutumiwa zaidi kusoma hisia za mteja juu ya bidhaa au huduma fulani, kupitia maandishi kwenye sentensi, na kwa kutumia makundi mawili tajwa hapo juu mifano yake huwa hivi:
(Picha kutoka mtandaoni)
Hizi aina mbili zinatumika kukufahamisha manyabiashara kuhusu bidhaa/huduma yako kwa kutambua ;
Je bei ya bidhaa yako iko sawa kuendana na kundi la wateja uliyowadhamiria?
Je unakidhi mahitaji ya wateja wako?
Je uamuzi wako wa kuwa na mawakala ni mzuri?
Kama unachapisha maudhui je yanawafikia na kutimiza lengo ulilokusudia?
Je ubora wa bidhaa uko sawa au kuna cha kuongezea?
Je ni wakati wako sahihi wa kuwa na tawi?
Je ni upande gani uongeze juhudi za kutafuta masoko?
Katika kutumia teknolojia ya aina hii mfanyabiashara unaweza kupata mtu aliyebobea katika maswala haya na kupangilia mitambo namna ya kufanya kazi kwa kadiri ya mahitaji yako, ila safari ya biashara hasa ujasiriamali ni kujifunza kila siku kuna majukwaa mengine hutoa mafunzo haya bure kukuwezesha kujifunza na kutengeneza mtambo wa majaribio na kuanza kukufanyia kazi.
Wanasema maisha ni safari ya udhubutu au hakuna kitu kabisa, hivyo kwa kasi ya teknolojia na mabadiliko yake mfanyabiashara huna budi kuikumbatia na kuitumia kwa manufaa ya biashara yako na kukupunguzia msongo wa “hapa na pale”.

- Mawakala wenu hawana huduma mbovu – HASI
- Mna bidhaa bora zaidi kushinda maduka mengine hapa jijini – CHANYA
- Huduma mbovu/mbaya- HASI
- Bidhaa bora- CHANYA