Ni swala dogo lakini linanisumbua akili.

Daddo

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2013
Posts
1,435
Reaction score
1,025
Habri wanajamvi. Mimi ni kijana aged 25 na miezi kidogo. Nimebahatika kuwa katika mapenzi na msichana mmoja hivi wa age ya 22 kwa sasa na tunapendana sana.Tulibahatika kupata mtoto wa kike ambaye sasa anagota miezi 18. Mwanangu na mama yake wanaishi kwao na mpenzi wangu japo kwao hawako safi kifedha ila kwakuwa yule ni mwanangu nafanya kila niwezalo asipate shida.
Tatizo langu ni kwamba mpenzi wangu anataka kwenda kusoma chuo flani hivi kwa hiyo mwanangu atatakiwa abaki nyumbani. Nyumbani kwetu wanang'ang'ania mtoto akake kule kitu ambacho wazazi wa mpenzi wangu nao wamekataa yaani wanataka abaki pale.
Mpenzi wangu mwenyewe ananiambia mazingira ya pale siyo mazuri kwa mtoto hasa kama yeye hatakuwepo japo na yeye anasema hakubaliani na mimi juu ya kumpekeka mtoto kwetu.
Kwa upande wa nyumbani sina wasiwasi na mazingira maana mbali na kwamba chakula siyo cha shida bali hata malazi ni ya uhakika kutokana na kwamba mbali na nyumba ya baba na mama mimi mwenyewe ninabanda langu la vyumba vitatu na kila kitu kipo ndani.
Shida ni kwamba mimi niko kikazi dar ila kwa sasa niko masomoni na nyumbani ni mkoani.
Naombeni ushauri nifanyeje juu ya hili. Kosa ambalo ninakiri ni kwamba mimi sijawahi kumpeleka mpenzi wangu nyumbani kumtambulisha zaidi ya kuwaonesha picha na hata kwa mpenzi wangu sijawahi kwenda kutambishwa japo wananifahamu kupitia picha zangu na mawasiliano ya kwenye simu. Hii yote ni matokeo ya ubusy nilionao katika mambo yangu. Naombeni ushauri hapa.
 
You need to settle the issue with your couple, ni rahisi mtoto kukaa kwenuwewe mwanaume, wewe pia ni rahisi ku convince wazazi wako kuliko yeye
 
You need to settle the issue with your couple, ni rahisi mtoto kukaa kwenuwewe mwanaume, wewe pia ni rahisi ku convince wazazi wako kuliko yeye

Its okay mkubwa ila tatizo haliko kwa wazazi wangu bali kwa wazazi wake maana wenyewe wanataka mtoto abaki kwao huku wazazi wangu wakidai atoke kule sasa imekuwa ni kasheshe yaani kila upande unavutia kwake sasa mimi ndiyo nachanganya na hali hiyo kibaya ni hili la mwenzangu kusema hakubali mtoto achukuliwe na huku japo mazingira ya kumwacha kule yeye mwenyewe hayaamini.
 
Kwani malezi ya mtoto unahisi ni chakula na mahali pa kulala tu kuna vitu vingi vinaitaji hasa uangalizi wa hali ya juu, ningekuwa mimi mtoto ningeenda nae chuo ningetafuta chumba na dada wa kunisaidia nikiwa darasani
 
pole sana hapo itabidi uangalie namna ya kufanya
 
Put you Foot down mkuu. Wewe ni mwanaume, mchukue mtoto wako mpeleke kwa wazazi wako. Wao ndio wanakuelewa na watasupport uamuzi wako kama wanavyokusupport maisha yako yote. Mama yako hawezi kumtesa wala kutomuangali mjukuu wako bana.
 
Kwani malezi ya mtoto unahisi ni chakula na mahali pa kulala tu kuna vitu vingi vinaitaji hasa uangalizi wa hali ya juu, ningekuwa mimi mtoto ningeenda nae chuo ningetafuta chumba na dada wa kunisaidia nikiwa darasani

Mkuu ningekuwa nasoma chuo cha hapa bongo ingekuwa rahisi inshort sipo tz kwa sasa.
 
Put you Foot down mkuu. Wewe ni mwanaume, mchukue mtoto wako mpeleke kwa wazazi wako. Wao ndio wanakuelewa na watasupport uamuzi wako kama wanavyokusupport maisha yako yote. Mama yako hawezi kumtesa wala kutomuangali mjukuu wako bana.

Nashukuru kwa ushauri ndugu lakini kama nilivyokwisha kuelezea tatizo halipo kwa wazazi wangu maana na wao ndicho wanacholilia kwamba mtoto wabakinaye lakini wazazi wa upande wa mwenzangu ndio wametia ngumu hawataki atoke.
 
mtoto ni wa kwako na anatakiwa awe mahali unapo paamin na utakapo mtunzia bila shida ambapo mi naona ni kwenu. Kubali kuonekana mbaya ila mtt wako awe mahali salama na pa aman
 
ebu acheni malumbano nyie, kwani kuna aliyesema mtoto si wake? cha muhimu huyo mama mtoto achague moja kusuka ama kunyoa. wewe ongea na mzazi mwenzio vizuri, kama hataki kumuacha kwenu na kwao mazingira hayaamini, anataka nini sasa? jibu atakalotoa ndo mlijadili km inawezekana ama la.
 
Fikiria kwanza jinsi ya kufanya we kama we, so unataka mtelemko kwa wadau umiza kichwa nyau wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…