Daddo
JF-Expert Member
- Jan 17, 2013
- 1,435
- 1,025
Habri wanajamvi. Mimi ni kijana aged 25 na miezi kidogo. Nimebahatika kuwa katika mapenzi na msichana mmoja hivi wa age ya 22 kwa sasa na tunapendana sana.Tulibahatika kupata mtoto wa kike ambaye sasa anagota miezi 18. Mwanangu na mama yake wanaishi kwao na mpenzi wangu japo kwao hawako safi kifedha ila kwakuwa yule ni mwanangu nafanya kila niwezalo asipate shida.
Tatizo langu ni kwamba mpenzi wangu anataka kwenda kusoma chuo flani hivi kwa hiyo mwanangu atatakiwa abaki nyumbani. Nyumbani kwetu wanang'ang'ania mtoto akake kule kitu ambacho wazazi wa mpenzi wangu nao wamekataa yaani wanataka abaki pale.
Mpenzi wangu mwenyewe ananiambia mazingira ya pale siyo mazuri kwa mtoto hasa kama yeye hatakuwepo japo na yeye anasema hakubaliani na mimi juu ya kumpekeka mtoto kwetu.
Kwa upande wa nyumbani sina wasiwasi na mazingira maana mbali na kwamba chakula siyo cha shida bali hata malazi ni ya uhakika kutokana na kwamba mbali na nyumba ya baba na mama mimi mwenyewe ninabanda langu la vyumba vitatu na kila kitu kipo ndani.
Shida ni kwamba mimi niko kikazi dar ila kwa sasa niko masomoni na nyumbani ni mkoani.
Naombeni ushauri nifanyeje juu ya hili. Kosa ambalo ninakiri ni kwamba mimi sijawahi kumpeleka mpenzi wangu nyumbani kumtambulisha zaidi ya kuwaonesha picha na hata kwa mpenzi wangu sijawahi kwenda kutambishwa japo wananifahamu kupitia picha zangu na mawasiliano ya kwenye simu. Hii yote ni matokeo ya ubusy nilionao katika mambo yangu. Naombeni ushauri hapa.