Ni takwimu za kutisha sana katika Mahusiano/Ndoa. Kuna jambo tunapaswa kujifunza tupende tusipende ama sivyo tutaangamia


Inawezekana pia wanaume wa Kitanzania wamekuwa na hulka ya kunyanyasa na ku dominate wanawake wasio na fursa, kutokana na kwamba sasa wanasoma na fursa, hizo fursa zinakuwa ni ngumu!
 
Siku hizi watoto/ vijana hawaandaliwi kuwa waume/ wake Bora. Hakuna kutayarishwa kuwa responsible, accountable na kujitambua. Tunajazwa uwe msomi, upate Mali, uwe na maisha Bora, uwe na vitu...
 
Wanawake uliyowataja hawana tatizo lolote. Tatizo ni tabia za mfumo dume tuliyonao na kwa wanawake wasomi wenye ajira na kipato kizuri hawaoni faida ya kukaa kwenye mahusiano yanyoendeshwa na mfumo dume. Hata hao ambao si wasomi au wenye kipato kidogo kuna wengine wako kwenye ndoa kwa sababu ya "economic insecurity". Kama si hiyo wangekuwa wameomndoka kwenye hayo mahusiano. Kwa kifupi mchawi si kisomo au kipato bali tabia za mfumo dume za wanaume.

Ndoa ni ya equal partners ikiendeshwa na mila, dini, na mapenzi. mapenzi yakiishaisha na kuanza ubabe, kwa nini mtu awe king'ang'anizi. Kuna wanawake wengi wanaishi katika mateso. Hao wasomi wanajuwa haki zao na pia hawaogopi kutoka kwa mwanaume kwa sababu wana uwezo wa kujitegemea.
 
Na hao wa kiume huwa wanafundishwa kwa malengo gani, mbona hatuoni wakivumbua cho chote?
 
Jamii imewekeza sana kwenye elimu dunia tunasahau kuwafundisha binti zetu na vijana wetu elimu ya kiroho.

Haya ni maneno mafupi sana kutoka kitabu kitakatifu Biblia lakini kwenye ndoa yana maana kubwa;

MATHAYO 19:6 "Kwa hiyo, wao si wawili tena bali mwili mmoja. Basi, alichounganisha Mungu, binadamu asikitenganishe"

MATHAYO 19:5 "Hii ndiyo sababu mwanaume atawaacha baba na mama yake na kuungana na mke wake. Na hao watu wawili watakuwa mmoja."

WAEFESO 5:28 "Vivyo hivyo waume wawapende wake zao kama miili yao. Anayempenda mkewe anajipenda mwenyewe."

WAEFESO 5:24 wake pia wanapaswa kuwatii waume zao kwa kila jambo

WAEFESO 5:33 "na mke naye ahakikishe anamheshimu mumewe."

WAEFESO 5:23 Kwa maana mume ni kichwa cha mke kama vile Kristo alivyo kichwa cha kanisa

MATHAYO 19:9 "Lakini haikuwa hivyo tangu mwanzo. Basi nawaambieni, yeyote atakayemwacha mke wake isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, akaoa mke mwingine, anazini.”

Kwa mume na mke Wakristo wakiishi kwa kutii hayo maneno watadumu katika ndoa. Haijalishi mke ana elimu nyingi au hapana.

NB: MUNGU SIKUZOTE HAKOSEI
 
Wanawake wa siku hizi hata usome maandiko huku unalia,hawaelewi.Siku wakiamua kurudisha akili zao vichwani ili zitumike kwa manufaa,watafanya hivyo.Wakiamua tu.
 
Haishi kitawa maana mnayoyapata kwenye ndoa anayapata huko kitaa bila tatizo. Hana stress kama wengi wetu humu
Hivi unaijua raha ya kupewa kero ndogondogo na mke unayeishi naye chumba kimoja tena kila siku?Huyo hajui raha ya kumuona mke kajinunisha bila sababu.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Na hao wa kiume huwa wanafundishwa kwa malengo gani, mbona hatuoni wakivumbua cho chote?
Wote hatuvumbui kitu!! Elimu yetu ni ya kukariri past papers na possibles!! Utavumbua nini??
but that's not what im trying to say it here either!
Namanisha kuwa , tofauti na wanawake , Hakuna mwanaume anaingia kwenye ndoa kwa mikakati kuwa azingue mbele ya safari na kupata Tangible investments, kupitia Talaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…