Ni tamaa za wahindi walioanza kuwa ceo wa makampuni ya tech au? kwanini sikuhizi software nyingi unalipia kila mwezi au mwaka badala ya moja kwa moja?

Ni tamaa za wahindi walioanza kuwa ceo wa makampuni ya tech au? kwanini sikuhizi software nyingi unalipia kila mwezi au mwaka badala ya moja kwa moja?

Kama mteja hata mimi nachukia hili ila ukiangalia upande wao inaleta maana.

Software hasa za kisasa zinazotegemea server zina gharama zinazoendelea baada ya mteja kuipata kwa hiyo kuuza kwa one time sale haileti maana kibiashara, siwezi kukuuzia app kwa mara moja kisha niendelee kuisupport na kuiboresha kwa miaka 5 ijayo.

Fikiria atafanyaje na wafanyakazi na gharama za biashara maana yake nikishatoa v1 nifukuze watu kazini mpaka tutakapoamua kutoa v2, vile vile kwa kuwa kampuni hizi hasa kubwa zinauza hisa mauzo ya mbele ni muhimu zaidi wawekezaji wanataka kuona huko mbeleni utauza kiasi gani kwa kuwaweka watu kwenye subscription hilo linakuwa rahisi zaidi kutabiri.

Pia hakuna mtu atakayelipia bei halisi wakiamua kufanya hivyo hata app ya $1 tunaipigia mahesabu utalipa $100 kwenda juu kwa lifetime v1 access ambayo inaweza kuacha kufanya kazi Google wakifanya update ya Android?
 
Hii ni opportunity KWAKO mkuu. Tengeneza alternative softwares, zenye performance sawa au better kuliko hizo za wahindi then zifanye ziwe na unlimited access after one time payment.
 
Back
Top Bottom