Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Si mara ya kwanza hili limefanyika, kwamba Polisi watamkamata mtu, watamuweka ndani, halafu akiwa ndani ndio wanaanza kujiuliza, sasa huyu tumfikishe mahakamani kwa kutumia vifungu gani vya sheria?
Ndio maana ni rahisi sana Tanzania kukamatwa na kupelekwa mahakamani, kuachiwa na hakimu, kisha polisi wakudake tena ukitoka tu mahakamani ili wakakubadilishie mashitaka
Hivyo wala hatushangai kwamba hawaoni hata aibu kutamka maneno haya kuhusu suala la kumkamata Dr. Slaa, "Ni sahihi daktari yupo, tuko naye na tumekuwa na mahojiano naye kwa baadhi ya mambo na mahojiano yetu yanakwenda vizuri kwa hiyo tunaangalia mifumo ya kisheria inatuelekeza nini cha kufanya naamini taarifa zaidi zitatolewa baadaye,”
Sasa hii inakuambia nini juu ya polisi wetu? Ni wazi wamejaa ujinga na ukihiyo! Wananikumbusha Mafarisayo waliokuwa wakimhoji Masiya ili atamke kitu cha kumfungulia mashitaka! Sijui kati ya Polisi wetu na Mafarisayo nani ni mwovu zaidi.