Ni tatizo kwenye maneno haya ya Kiswahili?

Ni tatizo kwenye maneno haya ya Kiswahili?

MWALLA

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2006
Posts
16,952
Reaction score
10,500
Kiswahili chetu kitakaa sawa lini?

Nashindwa kuelewa haya maneno MBUNGE, MBWA, MBU

Kwanini tusitumie au isomeke vizuri kwa kuandikwa M'BUNGE badala ya MBU-NGE ipi ni sahihi hapa na unaisomaje?
Au tuchukulie MBWA... Hii ukiisoma hivi naona inaka sawa Mmbwa badala ya MBWA, Mmbu badala ya MBU.

TUSAIDIANE KUBORESHA LUGHA YETU.
 
Ngoja tuwasiliane na BAKITA/TUKI,wao ndio wenye mamlaka hayo kisheria,tuone nao wanasemaje?.
 
Ngoja tuwasiliane na BAKITA/TUKI,wao ndio wenye mamlaka hayo kisheria,tuone nao wanasemaje?.

Vipi umeshafanya jitihada za kuwasiliana? Tumekaa mkao wa kusubiria urudi utwambie hao BAKITA wanasemaje.
 
Lazima kutambua kuwa kila lugha inakanuni za kimofolojia ktk maumbo ya maneno.mbunge, mbwa na nzi yako sawa.
 
Mkimaliza kuweka sawa kiswahili halafu msisahau na kiingereza ambacho maneno yake yanavyoandikwa ni tofauti na yanavyotamkwa.
 
mkimaliza kuweka sawa kiswahili halafu msisahau na kiingereza ambacho maneno yake yanavyoandikwa ni tofauti na yanavyotamkwa.

jadili chungu chako... Ucjadili ya jirani yako... Utaitwa mshakunaku mpekupeku
 
Mkimaliza kuweka sawa kiswahili halafu msisahau na kiingereza ambacho maneno yake yanavyoandikwa ni tofauti na yanavyotamkwa.

kweli aisee,mfano mtu anavyotamka neno ''gas''ni tofauti na linavyoandikwa.
 
Back
Top Bottom