Ni title gani ungekipa kisa hiki ambacho ni cha kweli

Ni title gani ungekipa kisa hiki ambacho ni cha kweli

BoManganese

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2017
Posts
980
Reaction score
2,679
Nawasalimu wanaJF basi ningependa niende moja kwa moja kwenye kisa hicho cha kweli kilicho tokea miaka ya nyuma.


Julia Pastrana ni mwanamke aliyekuwa na roho nzuri lakini alijulikana kuwa ni mwanamke mwenye sura mbaya sana, alizaliwa mnamo mwaka 1834 katika sehemu ya milimani nchini Mexico.

Tangu kuzaliwa kwake alipatwa na tatizo la nywele kukua kwa kasi hasa sehemu za usoni na kufunika sehemu zingine za mwili. Katika mazingira aliyokuwa anaishi watu walimuogopa na kumkataa wakimwita ni jitu la kutisha "monster".


main-qimg-4eb61d8b2c7660da31caa190d0d3d1c1.jpg

Julia Pastrana.


Kutokana na kukataliwa pale sehemu alikokuwa anaishi aliamua kutokomea kusikojulikana. Wakati akiwa njiani alikutana na kijana mmoja, kijana huyo alikuwa anafanya kazi katika kumbi za maonesho ya sarakasi hivyo alipomuona Julia na ulemwonekano wake wa kutisha aliona atafaa sana kwenye maonesho.

Julia Pastrana akapewa dili la kufanya kazi katika kumbi za maonesho, alikubali ingawa ilimuumiza na hakukuwa na namna nyingine ya kumuwezesha kuingiza kipato.

Uwepo wake katika kumbi hizo za maonesho ya sarakasi ulisababisha mafanikio makubwa kwasababu mapato yaliongezeka watu walikuwa wakilipa pesa ndefu kwenda kushudia binadamu wa ajabu anafanana na nyani au monster.

Kutokana na mafanikio hayo manager wa Julia katika maonesho hayo aliyekulikana kama Theodore Lent aliamua kumuona Julia, ilikuwa ni kitu cha kushangaza sana watu walijiuliza mwanaume anawezaje kumuoa mwanamke mwenye sura Kama ile. Harusi yao ilitrend sana kwa wakati kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari. "How could normal man marry a 135cm tall monster" vyombo vya habari vilihoji.

Baada ya muda Julia alifanikiwa kupata mimba na kuzaa mtoto wa kawaida kabisa lakini kwa bahati mbaya Julia Pastrana na mtoto wake walifariki dunia baada ya masaa 48 alipotoka kujifungua.

Lakini kujulikana kwake hakukuishia hapo kwasababu mme wake Theodore Lent aliamua kuuhifadhi mwili mwa mkewe Julia usiharibike baada ya kufa (mummifying) ili watu waendelee kushangaa mwili wa binadamu wa ajabu huku yeye akiingiza kipato kupitia maonesho hayo.

main-qimg-3185c809e7319b4634b85975423e3310.jpg

Mwili wa Julia uliotunzwa baada ya kufariki (mummified body of Julia Pastrana after her death)


Mwili huo uliibwa na watu wasio julikana mara nyingi hadi mara ya mwisho mwaka 2005 mwili huo ulipo patikana nchini Norway kwenye Dustin ya matakataka.

Hatimae baada ya miaka 150 mwili wa Julia Pastrana unazikwa kwa mazishi ya heshima kama walivyo binadamu wengine.


MWISHO...


CC: KENZY Behaviourist cariha Yna Bujibuji Mwifwa Sky Eclat Jane Lowassa Carleen miss chagga Mshana Jr Kichwa Kichafu Deejay nasmile linahbaby zagarinojo MalcolM XII Darmian Paula Paul Joanah Rowin adden rikiboy Extrovert Chizi Maarifa MO11 cutelove financial services

And so many others..
 
Julia pastrana,kibaya kilichojiuza.

Julia pastrana,mwanamke aliejizolea umaarufu kwa ubaya wa sura yake!.

Ubaya wa sura ulivyomneemesha Julia pastrana.
 
Kutana na Julia pastrana mwanamke mrembo aliyekonga nyoyo za wanaume mashababi.
 
Mother of evolution .

Evolution at its finest .

Love is a product of evolution.
 
Back
Top Bottom