Zote ni trekta bora. Mara nyingi ubora wa trekta unategemea na wewe mmiliki pia, kama hulitunzi na kuliheshimu, litaitwa marehemu kabla hata ya mwaka kuisha. Ngoja nikupe ufafanuzi mdogo wa matrekta ila kama ukihitaji zaidi ni pm nikupe namba yangu unipigie nikueleze kwa undani maana maelezo ni mengi na inchosha kuandika kwa kutumia simu.
1)Massey Ferguson(mf) hili trekta tangu enzi za mwalimu lipo na spare zake ni nyingi mno hata ukiwa mashamba ya ndani ndani sana utapata spare na mafundi kibao wanalijua hili. Ni trekta imara sana. Yapo yanayotoka England na mengine yanatoka Pakistan. Kama mfuko unaruhusu chukua ya England ni imara sana na bei ipo juu kuliko hayo ya Pakistan na spare nazo bei ni hivyo hivyo. Spare ya kutoka Uingereza huwa ni juu hata mara mbili ya spare ya kutoka Pakistan
2) John Deere(jd). Nalo ni zuri ila usichukue yanayotoka India si imara sana. Nafikiri haya pia yanatoka England au Marekani. Kwa ujumla Jd bei ipo juu hadi vipuri vyake pia vipo juu haijalishi imetokea nchi gani. Na upatikanaji wa spare Tz hapa ni wa shida na wanaoziuza wanaringa na bei inabadilika muda wote kwa sababu wanajua zipo chache. Mafundi wengi hawazijui hizi so likiharibika kupata fundi anaezijua kidogo huwa inasumbua.
3) New Holland ina sifa kama za mf japo lenyewe kwa hapa nchini si kongwe sana. Ila nalo ni imara sana na mafundi wapo wa kutosha. Spare zake ni ghali kulinganisha na mf ila zinapatikana karibia Tz yote.
ANGALIZO!
Nunua trekta kulingana na mahitaji yako na mazingira ulipo. Usinunue ili mradi uonekane na wewe unamiliki trekta litakushinda.
Matunzo ni muhimu sana lenyewe pia linahitaji matunzo kama vile unavyotunza vitz, vx, rav 4, range rover au ford ranger[emoji16]
Usinunue trekta kwasababu ya kampuni kujulikana sana, utalia sana pia
Sent using
Jamii Forums mobile app