Ni tukio gani la kusikitisha lililowahi kukuta ukiwa night club hadi leo hujasahau

Ni tukio gani la kusikitisha lililowahi kukuta ukiwa night club hadi leo hujasahau

Nilikuwa ninakojoa nje ya club sasa wakati ninataka kufunga zip likatokea kundi LA wadada warembo mmoja alinimulika na toch ya simu yake pale ktk zip wakaiona MASHINE yangu wakanidaka woote na kuniingiza ktk Gari lao nilikuwa Mpole Saana Kwa kuwa walikuwa warembo sikukukuruka nikajifanya mpole tu.Wakajifanya wAmeniteka wanataka huduma ya kusuguliwa duuuh niliwasugua kweli hadi SAA 4 asubuhi wako hoi ila walichanga wakanipatia wekundu 7 kama nauli.
[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Weekend moja nimejaribu kumtetea demu ambay alikua hataki kucheza na mhuni fulani ,dah nikajaribu kumtetea demu ,yani kilichogokea hapo wahuni wawili wametaka kuniua ,never again ,club sio sehemu za mchezo machizi ote wapo

Sent from my HTC Desire 310 using JamiiForums mobile app
 
Hii imenikumbusha kampala, kuna kijiclab kinavuma sana kinaitwa top club! Kuna machangudua balaaa! Basi nimefika pale ili nipate nyama choma na nile bear adhaa, ile natoka mida ya saa 7 hivi, kuna kahaba moja akajidai kanikubali, akawa ananipapasa papasa hivi, mara nikahisi ameingiza mkono kwenya mfuko wa mbele wa kijipensi changu, kuhamaki akazama mfuko wa nyuma na kuibuka na walete, aki pombe zilikata! Alivyogeuka sikutegemea, alitoka nduki kuelekea kwenye danguro lao, mimi nyuma mbio, kufika getini akachomoa hela iliyokuwa kwenye waleti na kirusha kwenye kingo ya ngazi, yeye akapotea na waleti haina kitu, kumbe mimi nimeona, kufika nikawahi zile pesa km zilivyo! Wenzake km 13 hawakujua ni nini nimechukuwa kwenye ngazi, walinidaka juujuu, nilihisi ndio mwisho wangu! Ila nilikukuruka kwa nguvu zangu zote, nikawszidi kisha nikaongoza kumfuata yule kahaba juu ghorofani, kufika kule watu wakawa wananishaangaa tu, nawaeleza jamani nimeibiwa, hawanielewi, kuna kahaba mmoja akanifuata akaniuliza, unataka wallet yako hutaki, nikamwambia nataka, ok basi toka nje utapata wallet yako, nikatoka nje, kweli ile nashangaanikaona waleti inarushwa toka gorofani, nikaichukuwa nikasepa kurudi hotelini. Uzuri hawakuchuwa hata senti tano, toka siku hiyo nimeapa top club sikanyigi!
 
Nakumbuka club maisha nmekula tungi lakutosha nafika toilet nkakutana na mchina nkaanza kumzingua na kumtukana,alinipiga pigo moja la kifuani nkajihis kufa,nikajikongoja kuwashtua washkaj ile wamemwona wakasepa kimyakimya
 
Nashukuru Mungu
Sijawahi enda Club
Sinywi pombe
Sivuti

Na vyote hivo sijawahi fanya
 
Nimekula starehe sana kwenye ma club...nakumbuka siku moja tulikua field dodoma tukaenda club maisha(sijui kama bado ipo) tulikua na mshkaji wangu muarabu mtata balaa basi kuna washkaji walizingua baada ya kuona madem zao wanamshobokea muarabu maana alikua na mpunga sio kitoto na madem wakija kwenye group yetu wanakula beer halafu hatuna tym nao jamaa zao waka mind aisee zilitembea nakoz ndani ya dkk 5 wale wasela wote chali..nikamwambia jamaa tuamshe hapa sisi wageni watatusubiri nje hawa..wkt tunatoka dem mmoja akasema hawezi kumuacha muarabu..tukasepa nae aisee hela ni shetani moja la ajabu sana aisee
Ila starehe na club zimetuondolea washkaji wengi sana kwasabau ya HIV na madawa ya KULEVYA wengi wamejifunzia kwenye ma club...R I P
 
Miaka hio Bado naenda club nikawa nimeenda Swizz pub kwa wale wa Tabata wanakumbuka ndio ilikua kipande maarufu Tabata na viunga vyake.
So enzi hizo I'm good kwenye kudance any kind of song Mzee.
One day kuna ile unakuta mjamaa sio club goer ila inabidi aje tuu club coz manze wake anakuja.
Basi Mzee hio njemba imekuja na demu wake kisu kweli kweli ila njemba ya hovyo hovyo tumbo ka fuko la taka Mzee yuko tungi plus kucheza ndio hawezi bora awe hajui. Demu anaonekana ana hamu ya kudance kweli kweli basi anakuja dance floor kwa kuibia ibia.
Ikafika stage DJ kaanza reggae raga na raga muffin mixer dancehall basi akawa kanifikisha. Tia style kibao pale mixer kalipso ya Uganda, kutaharuki binti kafutiwa na style zangu kaja tukaanza cheza. Ile namna wameimba navykenzo kamata chini kamatia chini tunaenda tuu.
Njemba wivu ukapanda tukasikia tuu chupa imefurumushwa bahati nzuri haikutupata ikavunjikia pembeni, kutahamaki Jamaa anataka anakwide nikampa push kaangukia pembeni. Akataka alianzishe Bahati nzuri Swizz kiwanja cha home kila mtu ananipata basi Jamaa akatulizwa.
Hapo manzi keshakimbia kenda kaa kwenye sofa.
Hili tukio huwa silisahau nikiwaza ile chupa ingenipata ingekuaje. au ningekua kiwanja ambacho si mitaa ya home ingekuaje?
Kaka miaka hiyo unayosema wewe ni miaka gani ambayo Navy kenzo walitoa kamatia chini. Maana hapa unavyoongea ni as if story ni ya 2005.
 
Ungetupa wallet yako na kweli waone umeitupa ungeelewa unaegombaniwa ni wewe au pesa yako.
Mimi sio type za wale wa kutembea na wallet MIMI muafrika natembea na hela zangu kwenye KIDONCHO

Unakijua!???
 
Niliingia night club kwa ajili ya kufanya show pamoja na freestyle nikiwa na washikaji zangu tukajikuta tupo wenyewe tu na DJ na mabaunsa.No mashabiki aseeee.....Niliumia sanaaaaa.
 
Niliutunza mkojo wa baunsa kisa eti nimemshika dem wake kiuno
 
Kaka miaka hiyo unayosema wewe ni miaka gani ambayo Navy kenzo walitoa kamatia chini. Maana hapa unavyoongea ni as if story ni ya 2005.
Hujaelewa mkuu. Hiko ni kibwagizo. Nimemaanisha tulikua tunacheza namkamatia chini tunapanda juu. Anakata kwenda chini namm namfata huko huko...

So ulitaka nisimulie tuu Kama nasoma risala kwa bashite? Bila kuweka nakshi?
 
Kipindi flani nipo ngudu, kuna bar moja inaitwa magreth ndo ilikuwa inafunguliwa.

baada ya kula na wenzangu viroba mimi vikanishindwa nikaweka senator. zilivyoissha hapo tukahamia safari club.

sasa kule ikawa mwendo ni kunywa tuu mpaka zikanishinda. nikaaga naenda choooni ili niwatoroke majamaa zangu nafika mlangoni hamadi wakaniambia huendi mahali turudi ndani. niliendelea kunywa mpaka nikawa hoi.

kurudi home nafika mtaa mmoja hivi nakutana na mmama mmoja hivi shemeji yangu. nikawaambia siwezi tembea. wakaniingiza gheto lao wale wamama wako kama wa nne hivi.

sasa nilichokumbuka wakaanza kunipaka rangi za kucha, mwingine ananipaka wanja, mwingine lipstic, mwingine ananitinda nyusi, mwingine ananivua jeans sijui walinibaka.

sasa asubuhi imefika bado tungi lipo kichwani nikaenda chooni kikaanguka uko, wakaja nitoa wakanifuta nguo. wakaona sijiwezi wakaniletea supu.

ile naenda nyumbani bado tungi lipo kichwani barabara nzima wananicheka na kunipiga picha. nafika nyumbani ndo naelewa walichonifanya.
 
Kweli hautasahau japo hiyo issue haikutokea club bali ilianzia club na kuishia nyumbani.
 
Back
Top Bottom