ningekuwa ndani ya ukawa ningeshauri haya
1.nawashauri ukawa wabadili mbinu wamsimamishe Tundu Lisu kugombea uraisi ili kudraw public attension ya usiniulize kwanini si dr. slaa
2.ufanyike mkutano mkuu wa vyama vyote vya ukawa na utangazwe nchi nzima na vuombo vote vya habari siku ya kumtangaza mgombea
3. itengenzwe ilani ya ukawa, na sera za ukawa zipitishwe siku hiyo
4. ilani ya ukawa ije na ajenda chache sana kama kumi na tano.tu ajena kuu ikiwa ni katba mpya, na muundo wa serikali tatu refer rasimu ya warioba
5. ili kuhakikisha ukawa ina kuwa na wabunge wengi na inakuwa na wigo mpaNA WA KUCHAGUA MAWAZIRI dr. slaa, lipumba mbatia na makaidi wagombee ubunge
6.hakikisha ukawa inasimamisha mgombea kila jimbo, na inaweka mawakala wa ubunge na uraisi, na baada ya matokeo fomu zote zipigwe picha au scan zitumwe kwenye server makao makuu kwa majumuisho
7. mgombea wa uraisi awe na kazi moja tu. kuinadi ilani yenye mambo muhimu kwa ufasaha na umakini ili hata mtu wa kawaida aweze kuelewa
8.wagombea ubunge na udiwani wao kazi yao iwe ni kufafanua sera kulingana na geographical location,
na kuna haja ya wagombea kupigwa msasa wa kuzijua sera kabla ya kampeni
9.ikiwapendeza ukawa wanaweza kuweka kwenye ilani yao mambo yafuatayo
1. kufufua mchakato wa katiba mpya -rasimu ya warioba
2.kuimarisha muungano wa jamuhuri ya tanzania kwa muundo wa serikali tatu
3. kubana matumizi ya serikali -kusitisha ununzi wa magari na maposho yasiyo na tija
5. kufuta misamaha ya kodi kwa makampuni makubwa pamoja na kufuta na kupunguza viwango vya kodi
kwenye bidhaa vifaa ya ujenzi kilimo viwanda na vyakula
6.kudhibiti matumizi ya dola na usafirishaji dola nje, pamoja na kupunguza inflation
7. kushusha kodi kwenye bidhaa za ujenzi
8. kutoa elimu bure mpaka chuo kikuu
9. kurudisha miswada yote iliyopitishwa kwa hati ya dharula ili ipite katika utaratibu wa kawaida ili ijadiliwe na bunge ipitishwe
10. kutengua mikataba17(MOU) ya kinyonyaji aliyoisani jk na wachina
11 kusitisha ujenzi wa bandari ya bagamoyo ili kuimarisha bandari ya dar tanga na mtrwara
13.kupitia upya mikataba ya madini,mafuta na gesi na nakuifuta ilie isiyo na maslahi kwa nchi
14 kurejesha nyumba za serikali