Subira the princess
JF-Expert Member
- Mar 3, 2018
- 3,474
- 3,744
Wasalaam.
Katika Serikali ya awamu ya 4 chini ya Jakaya Kikwete posho ya kujikimu safarini kima cha chini ilikua elfu 80 na cha juu ilikua 120,000 tofauti ilikua elfu 50.
Katika awamu ya tano chini ya Magufuli yeye hakuongeza wala hakupunguza aliacha kama ilivyo japo alitamani kuzifuta kabisa na kuzipeleka kwenye miradi ya maendeleo.
Katika awamu ya sita chini ya mama Mamia ameongeza kima cha chini kutoka 80 mpaka 100,000 na kima cha juu kutoka 120,000 mpaka 250,000 tofauti badala ya kupungua imepanda 130,000
Ukichunguza hivyo viwango unaona Serikali ya awamu ya 6 imeamua kufanya ukatili mkubwa kwa Watumishi wa Umma walio wengi na kuwaneemesha wachache wenye mishahara mikubwa, yaani mwenye nacho anaongezewa na asie nacho ananyonywa damu.
Inashangaza mwenye mshahara mdogo anaongezwa 20,000 na yule mwenye mshahara mnono anaongezwa 130,000 huu ni ubatili na ukandamizaji.
Hitimisho
Mtumishi wa Umma au raia anaeshangilia usanii na udhalimu huu akapimwe akili.