Joyce joyce
JF-Expert Member
- May 23, 2020
- 457
- 1,973
Wakuu, mwanzo nilidhani kuwa Uchaguzi huu utakuwa Uchaguzi mwepesi sana kwa CCM, nilidhani kuwa CCM itaenda kimteremko na nikafikia kutaka kukataa kwenda kufanya update zangu za kadi ya uchaguzi.
Nilihisi kuwa ni Uchaguzi utakaokuwa na wapiga kura wachache kuwahi kutokea nikadhani kuwa watu wameachana na issue za kwenda kupiga kura.
Lakini ninachokiona ni tofauti kabisa nilivyofikiria, inaonesha kuwa huuu Uchaguzi utakuwa Uchaguzi wa kuvutia na utakuwa Uchaguzi mzito kuwahi kutokea, ni Uchaguzi ambao unaonesha kuwa kutakuwa na makundi mawili hasimu kwa chuki kubwa, ni Uchaguzi ambao huenda ukamalizika kwa ishara isiyo nzuri.
Watu inaonekana wanaenda kupiga kura Kwa hasira na inaonesha kuwa huu ndio uchaguzi utakaochanganya wana CCM wengi na wapinzani Kwa kumpigia kura mpinzani.
Uchaguzi huu unaonekana kuwa wana CCM wengi wanaenda kupiga kura kwa upinzani kisirisiri, ni Uchaguzi utakaofuatiliwa na wakubwa wa nje kuliko chaguzi zote zilizopita.
Hii inaonesha kuwa kwenye siasa lolote linaweza tokea muda wowote, nimeanza kuona wale waliohamia upande wa pili wakijuta maaana kutokana na hali ilivyokuwa waliona Kabisa kuwa kwenye Uchaguzi hakutakuwa na upinzani ndio maana wakageukia upande ule.
Kuna kila dalili kuwa wanaCCM watajaa kwenye mikutano ya kampeni ila kwenye sanduku watapiga upande ule, inasemekana kuwa watu wameteseka sana na hiii awamu Lakini hawana pakusemea, nasikia wanataka kutolea hasira zao kwenye sanduku.