Uchaguzi 2020 Ni uchaguzi mgumu kutokea Tanzania na lolote linaweza kutokea

Unasema hivyo kutokana na watu unaowaona kwenye kutafuta wadhamini? Unadhani ni kipimo sahihi cha uchaguzi kua mwepesi au mgumu kwa CCM? Fikiria upya mkuu
Mimi binafsi naogopa hao watu!
Kwa uwingi wao wanaona wamesha shinda hata kama hawakupiga kula!
Hivyo akitokea mtu akisema mmenyang'anywa ushindi, sijui kitakacho Tokea!
Muda sasa nipo kwenye Kusali na Kufunga Kuombea Amani Taifa Letu ili tuenfelee kunywa ghahawa bila bughudha!
 
Nadhani 1995 ulikuwa hujazaliwa! Huo ndio ulikuwa mgumu! Huu ni mlaini ajabu
Mkuu ule Uchaguzi wa 2015 ulikuwa mlaini sana, watu wengi sana waligeuka wakamsupport magufuli kwa wingi mno, Watu wengi sana walibadili gia angani na kumsupport magufuli walidhani kuwa mambo yatakuwa sawa walimuunga mkono Kwa wingi Lakini watu wameumizwa sana na awamu hiii wakakuta waliodhani sio, mfano Nzuri tu ni humo CCM angalia akina makamba waliomuunga mkono, akina diallo walivyomuunga mkono akina kinana Lakini angalia maumivu waliyokutana nayo hao ni wanaccm vigogo wachache tu, huku chini ndio usiombe sasa hao wooote wanaenda kuungana na wa upinzani na raia wa kawaida ndio utajua wajua.

Kwa awamu hiii waliofaidhika nayo ni wale tu waliopata uteuzi pamoja na kile kikundi kidogo tu hata idadi Ya 10,000 hawafiki Halafu ujumlishe naa baadhi Ya wasukuma basi ndio maana ninasema utakuwa Uchaguzi Mugumu mno maaana CCM zaid ya nusu watamtosa, usiangalie kwenye majukwaa watafika huko kumlagai kutokana nahofu waliyonayo ila kwenye sanduku la kula watamtosa wengi mno
 
Mimi napenda pia uchaguzi huru, haki pamoja na uwazi.

Tatizo Tanzania hakuna chama cha 'maana' cha upinzani.

Utabiri wa kusema sijui uchaguzi utakuwa mgumu ni utabiri wa kujifariji tu, lakini ukweli kutokana na uzoefu wa chaguzi mbalimbali ni kwamba matokeo ya kura za upinzani kwa ngazi zote yatakuwa ni ya aibu kuwahi kutokea tangia mfumo wa vyama vingi uanzishwe.

Nguvu ya upinzani iliisha pale Cdm walipomuuzia Lowasa chama, sasa hivi wanavuna walichokipanda.

Dr Slaa aliondoka na roho pamoja na uhai wa upinzani.

Wa kulaumiwa wapo na wanajulikana kwa majina, lakini nashagaa watu bado wanazidi kuwashadadia badala ya kuwawajibisha!

Sasa upinzani wenye sura ya genge na u kanda kitakitiaje hofu ya uchaguzi chama chenye 'popularity'?

Tunataka uchaguzi utendewe inavyostahili, pasiwe na visingizio ili waliokisuuza chama kwa talanta waaibishwe na matokeo ya haki.
 
Unajifariji kwa kujidanganya Kijijini kwetu umeambiwa kuwa walikuwa wamebaki watatu Ccm juzi wamekubali kuwa hakuna kura Kwa Ccm na hao wengne ni viongox wa Ccm wa kijiji kitu ambacho haijawahi tokea wewe unakuja kujifariji hapa
 
Hata wewe unajifariji tu mkuu, kwa kuwa kila mtu ni shabiki wa upande wake, tuombe uzima Mungu atupe afya tufike hiyo October 28 kumaliza ngembe.

Baada ya uchaguzi tutaanza kufukua hizi thread kukumbushana.
 
M25 wamejiandikisha inasemekana. Mpaka hapo mshindi hajajulikana?
 
Joyce joyce,

Umeskia watu wanataka kutolea hasira zao kwenye box la kura. Pia umesema lolote laweza kutokea.

Naikutoe hofu, litakolotokea ni JPM kupita kwa kasi kubwa sana. Cha kusikia changana na akili yako. Wengi hawamjui tundu lissu. Membe wanamjua ila chama alichohamia hawakijui afadhali Chadema waliwahi kuiskia 2015 wakaipenda kwa sababu ya mwana CCM mwenzao Lowassa.

Asilimia kubwa huko vijijini hawamjui Lissu, membe ndio kabisaaa afadhali mara mia ya Prof. Muda wa kampeni hautoshi kuwatangaza. JPM amepita sana na anafahamika vyakutosha na anatajwa vya kutosha. Crowd kubwa huwa wanasikia upepo unapovuma na wanakwenda huko huko.

Ndio uchaguzi sio wa kuchukulia poa ila upinzani hauna nguvu ya kutosha kwenye uraisi. Unaoona wanawika mitandaoni ni wanamabadiliko wachache ambao wanapayuka wanaonekana wana nguvu kubwa lakini wenye nguvu kubwa hata humu hawamo.
 
Pita kwenye project za Magufuli , uliza mtu yeyete, watakuambia Magu forever.
Uliza Wapitanjia nani raisi wenu 2020?
Jibu watakuambia Magufuli simba wetu.
Nenda migodini kwa wachimbaji waulize Tanzanite inaenda kwa Upinzani au Magu?
Watakuambia chagua Magu.
Ukweli uko pale pale kwenye kazi nzuri za Magu.
Lisu amejihalibia kutukana tukana.
Wewe ni sawa na kiongozi , unaulizwa swali na mkazi wa Songwe, Magufuli amefanya nini
Unajibu amajenga flyover Ubungo.

Shenzy kabisaaa
 
Mkuu ule Uchaguzi wa 2015 ulikuwa mlaini sana, watu wengi sana waligeuka wakamsupport magufuli kwa wingi mno, Watu wengi sana walibadili gia angani na kumsupport magufuli walidhani kuwa mambo yatakuwa sawa walimuunga mkono Kwa wingi Lakini watu wameumizwa sana na awamu hiii wakakuta waliodhani sio, mfano Nzuri tu ni humo CCM angalia akina makamba waliomuunga mkono, akina diallo walivyomuunga mkono akina kinana Lakini angalia maumivu waliyokutana nayo hao ni wanaccm vigogo wachache tu, huku chini ndio usiombe sasa hao wooote wanaenda kuungana na wa upinzani na raia wa kawaida ndio utajua wajua.

Kwa awamu hiii waliofaidhika nayo ni wale tu waliopata uteuzi pamoja na kile kikundi kidogo tu hata idadi Ya 10,000 hawafiki Halafu ujumlishe naa baadhi Ya wasukuma basi ndio maana ninasema utakuwa Uchaguzi Mugumu mno maaana CCM zaid ya nusu watamtosa, usiangalie kwenye majukwaa watafika huko kumlagai kutokana nahofu waliyonayo ila kwenye sanduku la kula watamtosa wengi mno
Wewe unaota tu, JPM anapendwa ajabu. Siasa za Tanzania wewe ni mgeni wazo
 
Lissu amekuja kubadilisha kabisa upepo wa siasa za Tanzania, jamaa walijiamini wakadhani wameshashinda hata kabla ya kura kupigwa, sasa inawalazimu warudi kwenye drawing board waanze kujipanga upya.
 
Kuna mambo mengi Sana ndugu yanayoonesha

1. Mitaaani watu wanasema chini kwa chini kuwa watapiga upinzani

2. Vijijini wanasema kuwa wao ni upinxani

3. Watumishi wanasema chini kwa chini

4. CCM wenyewe huku chini wanaapa kuwa watapiga upinzani

5. Wafanyabiashara hivyo hivyo

6. Wakulima hivyo hivyo

Angalia kile kitendo cha kule Zanzibar cha kulazimisha watumishi kuungana kwenye mkutano wa mwinyi ni ishara

Lakini hata hiii idadi kubwa inayojitokeza kwenye mikutano Ya Lissu ni ishara kubwa mno, minongono pia, na hofu unayoiona Kwa Ccm Kwa sasa kila mahali ni ishara Mkuu na hizo huwa ndizo ishara zinazojulikana.
Kila kitu kinasemekana je wewe unasemaje?
 
Mkuu ule Uchaguzi wa 2015 ulikuwa mlaini sana, watu wengi sana waligeuka wakamsupport magufuli kwa wingi mno, Watu wengi sana walibadili gia angani na kumsupport magufuli walidhani kuwa mambo yatakuwa sawa walimuunga mkono Kwa wingi Lakini watu wameumizwa sana na awamu hiii wakakuta waliodhani sio, mfano Nzuri tu ni humo CCM angalia akina makamba waliomuunga mkono, akina diallo walivyomuunga mkono akina kinana Lakini angalia maumivu waliyokutana nayo hao ni wanaccm vigogo wachache tu, huku chini ndio usiombe sasa hao wooote wanaenda kuungana na wa upinzani na raia wa kawaida ndio utajua wajua.

Kwa awamu hiii waliofaidhika nayo ni wale tu waliopata uteuzi pamoja na kile kikundi kidogo tu hata idadi Ya 10,000 hawafiki Halafu ujumlishe naa baadhi Ya wasukuma basi ndio maana ninasema utakuwa Uchaguzi Mugumu mno maaana CCM zaid ya nusu watamtosa, usiangalie kwenye majukwaa watafika huko kumlagai kutokana nahofu waliyonayo ila kwenye sanduku la kula watamtosa wengi mno
Kinachotakiwa ni kujaza mikutano bila kujali wanaojaza watapiga kura au la na wakati wa kutangaza matokeo aliyeshindwa asiweze kuingiza watu barabarani.
 
Unajifariji kwa kujidanganya Kijijini kwetu umeambiwa kuwa walikuwa wamebaki watatu Ccm juzi wamekubali kuwa hakuna kura Kwa Ccm na hao wengne ni viongox wa Ccm wa kijiji kitu ambacho haijawahi tokea wewe unakuja kujifariji hapa
Acha utoto ww kwamba kila mtu alipitiwa na kuambiwa hamna kuchagua ccm.... Kura ni siri ya mpigaji kumbuka hilo... Na u have a work to do kushawish watu kumpigia lisu kura kama mnataka awe raisi..... Naona unaact kama nabii vile
 
Back
Top Bottom