Uchaguzi 2020 Ni uchaguzi mgumu kutokea Tanzania na lolote linaweza kutokea

Joyce joyce

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2020
Posts
457
Reaction score
1,973
Wakuu, mwanzo nilidhani kuwa Uchaguzi huu utakuwa Uchaguzi mwepesi sana kwa CCM, nilidhani kuwa CCM itaenda kimteremko na nikafikia kutaka kukataa kwenda kufanya update zangu za kadi ya uchaguzi.

Nilihisi kuwa ni Uchaguzi utakaokuwa na wapiga kura wachache kuwahi kutokea nikadhani kuwa watu wameachana na issue za kwenda kupiga kura.

Lakini ninachokiona ni tofauti kabisa nilivyofikiria, inaonesha kuwa huuu Uchaguzi utakuwa Uchaguzi wa kuvutia na utakuwa Uchaguzi mzito kuwahi kutokea, ni Uchaguzi ambao unaonesha kuwa kutakuwa na makundi mawili hasimu kwa chuki kubwa, ni Uchaguzi ambao huenda ukamalizika kwa ishara isiyo nzuri.

Watu inaonekana wanaenda kupiga kura Kwa hasira na inaonesha kuwa huu ndio uchaguzi utakaochanganya wana CCM wengi na wapinzani Kwa kumpigia kura mpinzani.

Uchaguzi huu unaonekana kuwa wana CCM wengi wanaenda kupiga kura kwa upinzani kisirisiri, ni Uchaguzi utakaofuatiliwa na wakubwa wa nje kuliko chaguzi zote zilizopita.

Hii inaonesha kuwa kwenye siasa lolote linaweza tokea muda wowote, nimeanza kuona wale waliohamia upande wa pili wakijuta maaana kutokana na hali ilivyokuwa waliona Kabisa kuwa kwenye Uchaguzi hakutakuwa na upinzani ndio maana wakageukia upande ule.

Kuna kila dalili kuwa wanaCCM watajaa kwenye mikutano ya kampeni ila kwenye sanduku watapiga upande ule, inasemekana kuwa watu wameteseka sana na hiii awamu Lakini hawana pakusemea, nasikia wanataka kutolea hasira zao kwenye sanduku.
 
Tume huru ya uchaguzi ndo muhimu
Usitegemee tume Mkuu, wewe jitokeze Kwa wingi Sana weka mikakati ya kulinda kura, hiyo tume kuna Wakati unafika inashindwa kuchakachua, mfano angalia Uchaguzi wa 2010 kule nyamagana kwa Wenje alivyoshinda walifanya kila namna, akini walishindwa kwa sababu kura zilipigwa kwa wingi sana upande wa Wenje.
 
Sawa nitatekekeleza
 
CHADEMA bado sana
Unajua hayo huwa yanafanywa na wananchi mfano Kwa Hali inavyoonekana Uchaguzi wa Mwaka huuu wananchi wanaenda kujiongoza wenyewe tofauti na miaka Ya Nyuma ambapo mbowe ndio Alikuwa anaoganaize kila kitu Kwa sasa ni wwenyewe.
 
Unasema hivyo kutokana na watu unaowaona kwenye kutafuta wadhamini? Unadhani ni kipimo sahihi cha uchaguzi kua mwepesi au mgumu kwa CCM? Fikiria upya mkuu
 
Unasema hivyo kutokana na watu unaowaona kwenye kutafuta wadhamini? Unadhani ni kipimo sahihi cha uchaguzi kua mwepesi au mgumu kwa CCM? Fikiria upya mkuu
Kuna mambo mengi Sana ndugu yanayoonesha

1. Mitaaani watu wanasema chini kwa chini kuwa watapiga upinzani

2. Vijijini wanasema kuwa wao ni upinxani

3. Watumishi wanasema chini kwa chini

4. CCM wenyewe huku chini wanaapa kuwa watapiga upinzani

5. Wafanyabiashara hivyo hivyo

6. Wakulima hivyo hivyo

Angalia kile kitendo cha kule Zanzibar cha kulazimisha watumishi kuungana kwenye mkutano wa mwinyi ni ishara

Lakini hata hiii idadi kubwa inayojitokeza kwenye mikutano Ya Lissu ni ishara kubwa mno, minongono pia, na hofu unayoiona Kwa Ccm Kwa sasa kila mahali ni ishara Mkuu na hizo huwa ndizo ishara zinazojulikana.
 
Umesikia takwimu za NEC lakini? Kwamba kwenye daftari la kudumu kuna voters 29mil.!!! Wewe umeamini? Inamaana Tz tupo karibia wtu 75mil? Nakuhakikishia wapiga kura hawazidi 20mil. Mazingira hatarishi hayo

Umemsikia KM wa Chama kuhusu incumbency advantage? Kwamba kwa waliopo madarakani kushindwa uchaguzi ni uzembe wao? Unadhani anazungumzia ubora wa sera na huduma kwa wananchi?

Kuhusu Zanzibar kwani wewe ni mgeni wa chaguzi za huko? Kwenye mpira tunasema ngoma ilishavuka mstari wa goli lakini mara zote refa anakataa kuweka mpira kati kwa shinikizo la kibabe la timu iliyofungwa!

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 
Hiii Ya idadi nimekuelewa Kwa asilimia Mia hili ni gori la mkono kubwa Sana kuna kumi imewekwa pale na ndio maanaa wanajiamini Lakini upinzani unatakiwa kutafuta suruhishi na kuona Namna Ya kufanya mapema iwezekanavyo
 
Nimeongea na mtendaji wa kata mmoja leo amesema unachosema.

Wala sio mtu wangu wa karibu lakini tulipoanza stories za hali ya maisha...alirukia kwenye uchaguzi. Akasema hata amini atakachokipata kwenye kura safari hii. Na alinihakikishia wafanyakazi wengi wana mafundo watakayoyamalizia kwenye kura.
 
Nyie ndio mliompoteza mzee wa watu Kwa maneno haya sasaanahangaika jamani mlikuwa mnamwambia hivyo hivyo kuwa upinzani umeishakufa daaah rudisha hela za mzee wa watu.
 
Ndicho kinachoenda kutokea Mkuu, watu wengi mno Na Kwa taarifa yako hata kinana Yule atapiga Kwa lisu huo ndio ukweli nakuhakikishia lisu atapata kura nyingi toka Kwa wanaccm kuliko za watu Wa kawaida.
 
Kumbe kumwambia mtu anatawala bila kuzingatia sharia au katiba nia matusi? Kubambikia watu kesi ni matusi? Kumzuia asipate hela ya matibabu ni matusi?

Ukweli umeingia huo ...na maumivu ya ukweli mnayoyapata mnaona kama mnatulanwa.
 
Halafu kuna kitu MUNGU akipanga hata uwe na siraha hata useme kuwa utachakachua yeye anakuwa na njia mandala kikubwa wanasiasa wawe makini na matendo yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…