BUSH BIN LADEN
JF-Expert Member
- Mar 16, 2019
- 8,447
- 19,425
Habari wana jukwaa? Naomba niende moja kwa moja kwenye mada.
Leo nikiwa naangalia mapokezi ya Rais Kagame wa Rwanda nchini, TBC walirusha kipindi flani cha historia kikionyesha ziara ya Mwalimu Nyerere nchini Rwanda enzi za Rais Habyarimana.
Katika ziara yake hiyo, mwalimu alitembelea kiwanda cha bia inayotokana na ndizi ila pia akatembelea eneo moja linaitwa Ruhengeri ambako kuna bonde moja lina udongo ambao ukikaushwa unatumika kama chanzo cha nishati.
Nimejaribu kutafuta mitandaoni huu ni udongo gani nimekosa majibu ila pia nikahisi itakuwa makaa ya mawe ila hakuna ripoti popote nimeipata inayoonyesha uwepo wa makaa ya mawe nchini Rwanda.
Kwa anaeweza kuwa na ufahamu tafadhali naomba kujua huu ni udongo gani na kama unaweza kupatikana Tanzania.