Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
NI UGAIDI JESHI KUPIGA WANANCHI WASIO NA HATIA KISA WANAONYESHA HASIRA ZA MWENZAO/WENZAO KUDHURIWA NA MTU/KIKUNDI FULANI.
Anàandika, Robert Heriel
Kamanda wa Tibeli.
Kuna ile tabia ambayo sasa nadhani imezoeleka ya kulichafua jeshi letu au baadhi ya wanajeshi wasiowaadilifu kuchafua kazi ya uanajeshi kwa kufanya matendo ya kidhalimu, matendo yasiyo ya haki. Jambo ambalo kwa sisi Watibeli halikubaliki, na tunalipinga kwa kinywa kipana pasipo kumung'unya maneno kuwa tabia hizo ni mbaya na lazima zikemewe na watu wote waungwana na waadilifu.
Moja ya tabia hizo ni pamoja na tabia ambayo nimeihusisha na ugaidi.
Tabia ya kupiga na kudhuru wananchi wasio na hatia kisa na mkasa ati kulipa kisasi cha kijinga baada ya mwanajeshi kupigwa au kudhuriwa na Rais fulàni au kikundi fulani cha Watu.
Yaani ati mimi leo niingie kwenye mgogoro na jirani yangu mjeshi, au nipo Bar nipo kwenye ishu zangu za starehe mara nimeingia mgogoro na mjeshi tukazichapa na nikampiga au kumdhuru. Ati kinachofuata ni eneo hilo au mtaa ninaoishi kupokea kichapo hata kwa wasiohusika. Huo ni ugaidi, ukatili, na udhalimu.
Wanajeshi tunajua wazi kuwa nidhamu na uadilifu ndio kanuni zinazotuongoza. Nidhamu ni kujiheshimu, kuheshimu muda, kuheshimu Watu wakubwa kwa wadogo. Uadilifu ni kutenda mambo kwa weledi na kwa Haki.
Mwanajeshi halisi na muadilifu hawezi kupiga raia asiye na hatia ati kisa kulipa kisasi cha mtu au kikundi fulani kilichomdhuru mwanajeshi mwenzake. Huo sio uadilifu. Huo sio uanajeshi.
Hiyo kasumba iondoke. Hiyo tabia ikemewe. Wanajeshi ni Vijana wetu, Baba zetu na wajomba zetu, Dada, mama na shangazi zetu. Heshimuni maadili ya kazi yenu. Hiyo ndio namna ya kulifanya jeshi letu lipendwe na lilinde heshima yake.
Najua wapo wanajeshi waungwana na waadilifu ambao wanaelewa kile ninachokizungumzia.
Mwanajeshi lazima uelewe kuwa unapokuja huku uraiani wewe ni raia tuu kama raia wengine. Lazima ufuate sheria za nchi na uheshimu Watu ili na wewe uheshimiwe.
Tena Raia huwapa upendeleo kwa sababu wanajua umuhimu wa kazi yenu. Lakini tabia ya kulazimisha upendeleo na heshima ndio inayoleta matata na changamoto huku mitaani.
Unaleta ubabe na dharau kwa kinga ya jeshi. Yaani unalitumia jeshi vibaya. Huo sio uadilifu.
Niheshimu uheshimiwe. Elewa kuwa utakapoingia kwenye mgogoro na mtu utaingia wewe kama wewe na sio jeshi. Kulitumia jeshi kwenye shughuli zisizoza kiadilifu ndiko kunakolichafua jeshi.
Tabia hiyo ikemewe. Na wenye tabia hizo wachukuliwe hatua kali naza dhahiri ili iwe fundisho katika nchi.
Nipumzike sasa.
Sabato njema.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam