Mtayarishaji
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 291
- 198
Siku za hivi karibuni binti yake Rais Donald J Trump wa Marekani ajulikanaye kwa jina la Tiffany Trump amekuwa akionekana sana akiwa karibu na kijana wa Kilebanon ajulikanaye kwa jina la Michael Boulos na ukaribu huo moja kwa moja umetafsiriwa kuwa ni uhusiano wa kimapenzi.
Kuna kipindi wawili hawa walionekana wakiwa matembezeni nchini Ugiriki, Falme za kiarabu/Dubai na hata katika viwanja vya mbali mbali vya starehe katika majiji ya Marekani.
Michael Boulos ni mtoto wa bilionea tajiri wa Kilebanon ajulikanaye kwa jina la Massad Boulos mmiliki wa makampuni ya Boulos Enterprises na SCOA Nigeria yaliyopo nchini Nigeria yanayojishughul
isha na uuzaji wa magari, Vipuri vya magari na ujenzi nk.
Massad Boulos na mwanaye ni miongoni mwa wanaokiunga mkono chama cha Marada kilichopo nchini Lebanon ambacho ni rafiki wa wanamgambo wa Hizbollah wanaoitwa magaidi na Marekani na washirika wake kama Israel, Saudi Arabia nk.
Nitastaajabu sana endapo Marekani haitamuweka Tiffany Trump na mpenzi wake huyo kwenye orodha ya magaidi. Kama sio hivyo basi itakuwa Tiffany Trump ni jasusi anayekusanya taarifa za siri za Marada na Hizbollah kupitia Michael Boulos zitakazousaidia utawala wa baba yake.
Credit: Suleiman Bin Majid