Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa faida ya wanajamvi.Habari wana Jamvi.
Nna Mtoto wa Kiume Umri miaka miwili na nusu 2.5 sijamfanyia tohara na niliacha kumfanyia mapema kulingana na mila na desturi za kwetu maana mie Baba ake nilifanyiwa nikiwa kidato cha pili.
Sasa leo mtoto amenishtua kidogo ametoka kuogeshwa akamwambia Mama ake
''Mama nataka kukata dudu yangu"
tukatafsiri kuwa majirani wanaomzunguka a watoto anaocheza nao wote wamekatwa yaani wamefanyiwa tohara tukahisi labda watoto wenzake wamemwambia lazima akatwe.
je akiendelea kuachwa hivyo hivyo hakuna siku tunaweza pata amejikata dudu yake?
je Umri sahihi kiafya ni upi hasa?
Habari yako mkuu, ushauri wangu ni kwamba kumfanyia tohara mapema ni bora zaidi,Kwa hiyo Mkuu unashauri nisubiri akue kwanza?wasiwasi wangu anaweza kudanganywa nikapata amekata dudu yake kama alivyosema jana
Upo sahihi sanaKwa maoni yangu.. Usimfanyie mtoto tohara akiwa Mdogo sana.. Maana hizo sehem ndo kwanza zinakuwa.. ! Na kama unavyojua kukata dudu (kama alivyosema dogo) kuna maumivu sana.. ! Kiasi kwamba husababisha kufa kwa cells ambazo ni muhimu kwa ukuaji wa dushe la mtoto, due to high stimulation ya nerves zake... Mwishowe mtoto huwa na kibamia... ![emoji41]