Ni uongo gani uliwahi kusingiziwa na ukakugharimu sana japo haikua kweli?

Ni uongo gani uliwahi kusingiziwa na ukakugharimu sana japo haikua kweli?

Nelson Kileo

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2011
Posts
3,053
Reaction score
3,259
Kuna visa fulani hivi mtu anakusingizia jambo la uongo kabisa na akalitengeneza linaonekana kweli kabisa kwa upande wa pili na kuleta mtafaruku mkubwa unafikia hatua ya kuharibu hata Undugu Kazi, Ndoa, ama Urafiki kabiaa.

Kipi kisa Chako? Ni kwa namna gani au ukubwa upi kimekuharibia katika maisha yako?
 
Shuleni walinisingizia kuwa Mimi nimeenda kwa afsa Elimu kiwachongea walimu kuwa hawafundishi basi walimu woote pale shule wakajenga chuki na Mimi wakaanza kusetle mipango ya kunifukuzisha Shule ingawa walishindwa ila wengine walianza kukagua notice ambazo hata sijui waliziandikia wapi

Basi Kuna mwalimu mmoja mpenda sifa alinipiga Sana na fimbo mpaka akanivunja kiganja aisee iliniuma Sana na sitamsahau mwalimu yule wa civics popote pale ulipo nakuombea mabaya daima
 
Kusingiziwa namgonga mpangaji mwenzangu.. Hali iliyopelekea nikimsalimia mme wake haitikii
 
Hayasemeki...

Aisee unaweza kufa kihoro ..au kuwa katili wa kutupa na visasi vya kuua!

Binadamu ni zaidi ya wanyama... ..

Unatengenezewa mazingira ..unadhulumiwa.
Unaumizwa..unaachwa.. na hao hao wanakubambikia kesi na unakwenda jela..na wanakutoa baada ya miaka ila kwa masharti maalum ..laa sivyo utaozea jela!
 
Kuna visa fulani hivi mtu anakusingizia jambo la uongo kabisa na akalitengeneza linaonekana kweli kabisa kwa upande wa pili na kuleta mtafaruku mkubwa unafikia hatua ya kuharibu hata Undugu Kazi, Ndoa, ama Urafiki kabiaa.

Kipi kisa Chako? Ni kwa namna gani au ukubwa upi kimekuharibia katika maisha yako?
Sikumbuki. Nikikumbuka tu ntaleta script
 
Niliwahi kusingiziwa na boya mmoja hivi eti nimepanga mawe kwenye reli yale majamaa yanayopita na kiberenge yamevurugwa kinoma yakanibeba mkuku mkuku kunipakia niende nao wanakoenda ile najieleza ni kama vile hawanisikii. Daah nililia kinoma..
 
Ni kweli,enzi niko shule ya msingi miaka ya 80 nikapangwa dawati na Asunta na Mgenivisu vikali kweli,
Asunta mweusii black beauty,mgeni mweupee maana ni mbulu yule.
Tunakaa watatu kwenye dawati.
Mjinga mmoja Gerlad na wivu wake kaandika barua ya mapenzi kaitupa karibu na ofisi ya waalimu.
Bahati mbaya zaidi maza ni mwalimu shule hiyohiyo.
Nikachapwa fimbo 3 3 na walimu wote wako 15 hivi.
Haya maza nae akabeba hiyo barua apeleke home kumwonyesha mdingi.
Mdingi nae ana msala wake siku2 hajalala mle ndani..
E mungu kupewa ile kesi yangu,nilipigwa mimi mpaka nikazimika na nikanginizwa na taulo juu ya dari mpk nikakata moto.
Barua sijaandika mimi.
Mi nilipopata nguvu huyo Gerald tulichomrudishia.
Hawezi kusahau.
 
Dah sitaki hata kukumbuka hilo tulio ila nililipa kwa kumpa kilema cha maisha
 
Back
Top Bottom