Ni upuuzi mtupu kumpigia kura Idris na Miss World Tanzania

Ni upuuzi mtupu kumpigia kura Idris na Miss World Tanzania

wabongo kwa kujishaua,mbona ccm wamegawana hela zenu za kujengea maabara na bado mnapiga kura huku vijasho vya kwapa vinawatoka,kama una usingizi lala bhana tutolee upuuzi wako hapa
 
Faiza foxy kipi bora kuwapigia kura ccm ambao kila kukicha serikali yao na wanachama wao ni mafisadi na wahujumu uchumi au kumpigia kura idriss ambae amekwenda kujitafutia maisha yake kwa namna anayoamini itamtoa katika maisha ya kimasikini?

Tanzania hakipigiwi kura chama, anapigiwa kura mgombea. Watu huchaguwa mtu ndiyo maana huwa kuna kampeni za wagombea na mfano mzuri ni Slaa, alishindwa kura za maoni CCM akaondoka na akachaugliwa upinzani, jimbo hilo hilo.

Unavyoongelea maisha unaonesha ni mtoto mdogo na usiyeyajuwa maisha bado, kutoka kimaisha kwa kwenda uchi? nyie ndiyo mnadanganyika na kuuza thamani yenu ya ubinaadam eti kwa kuwa "utatoka" kimaisha.
 
Maana naona siku hizi watu tunahimizwa katika Media zote as if ni sahihi kufanya hivyo coz mi sioni yanatufundisha chochote katika maisha zaidi ya upuuzi mtupu. Kama vipi nendeni mkawaombee kura kwa wahuni wenzao, shwain!

Wanaoungana nami kwenye hili leteni michango yenu hapa. Na tupinge mashindano ya kipuuzi kama haya nchini kwetu.

Baadhi watanzania wanaakili za kushikiwa, upuuzi na ushenzi ndo wanashabikia, wale watu ambao mawazo yao yangeiendesha nchi vizuri hayadhaminiwi ila wape ujinga kama huo BBA, OK, Miss matakataka, na upuuzi n.k

Prof. Wa chuo kikuu akishauri jambo la maendeleo ya nchi na jambo hilohilo likashuliwa na either Masanja mkandamizaji au Wema Sepetu au msanii yoyote wasiojua hata maana ya maendeleo basi, wa tz walio wengi they will bear attention to these wasanii.

Ndo maana wenye elimu hawadhaminiwi bali wenye upuuzi.

Mfano, katika hali ya kawida Komba muimba taarabu na kwaya anaweza kukosoa kazi za kisomi za judge Warioba?

Bungeni wamejaa akina Komba unategemea nn kama si kuendelea kuangalia BBA na kupigania hata na ss tuyaandae.

Oòoo Tanzania umekosa nn mpaka ukapata kizazi kama hiki?
 
Kuanzia huyo Daiomnd wao..,walohangaika kumpigia kura wote ni wapuuzi..,yaan mtu badala ya kufanya mambo ya msingi unakaa na kupigia kura uhuni wa Big Brother..au unampigia kura yule muhuni Daimondi..ni upuuzi uliopitiliza...na hivi vyombo vya habari badala ya kuhimiza watu wakajiandikishe kupiga kura kuamua maisha yao, mnahimiza kuwapigia kura wafuska..hatari kubwa..mtu utakuta mishipa ya shingo inamtoka kabisa kwa sababu ya Daimond..mi mke wangu nshamwambia siku nkimsikia n mambo ya daimond naenda kwa babake kudai mali yangu..sitaki upuuzi nyumbani kwangu.

Hahahaa haaaa uwiii Yaani nimecheka jamani!

Samahani nine quote post ndefu
 
Big up Idriss watanzania tupo na wewe na tutahakikisha unarud na kitita cha mshindi.ukiona hupend game kaa pemben
 
Hebu nisaidie kuna mtanzania mwenzetu dola laki 3 inamchungulia na kitu pekee kati yake na hiyo pesa ni kura yangu. Je ni bora nimnyime kura abaki maskini kisa alikaa uchi au kumpigia kura achukue ma $$$ halafu tumkeme badae.
Kula like yangu mkubwa,vyovyote vile ilivyo tuangalie finally anapata nn na kwa kiasi gan pesa atakayopata atainvest na kuajiri watanzania wangapi au kwa kiasi gan ataiweka hiyo pesa kwenye mzunguko na kufaidisha watanzania walio wengi
 
mnaponda BBA mnatetea ufisadi wengine hapa daah!
what a shame!!
 
Hamna lolote yatakiwa pesa yake, the more you vote the mor you're making someone rich...lol. Huwa sipendi hizi programmes za kuvote shuwain! Wakishakuwa celebrity....hata attitudes zinachange.

Yani ni sawa na kupiga kura ya uraisi halafu kesho wewe unamuita bwana muzee lol
 
happiness wangu nimempigia kura mbaya,ni huyu nimempenda nikafanya hivyo,kama ww hupendi acha!!huwez ukalazimisha msimamo wako ufuatwe na kila mtu!!!
 
sipigii kura CCM tu ndio takataka to me...ila yotee napigia tu Lol
 
Naam, ni upuuzi usio na mfano. Kati ya civilization za mwanzo kabisa kwa binaadam ni pamoja na kujuwa kujistiri tupu zake na kuvaa nguo, leo tukapigie kura wavuwa nguo na watembea utupu kwa makusudi kabisa wakijianika bila kujali chochote.

Eti maendeleo! Khaa! kama si ujinga huo ni nini?

Bora kupiga kura kwa big brother kuliko kuwapigia kura mafisadi walio laaniwa wa ccm shenzy taipu.
 
Upuuzi huo hauiishii katika kupiga kura tu bali hadi kufisidi mitizamo ya kimaisha ya vijana wengi wasiojitambua
 
Dah pesa! mpaka mtu ukae uchi ndio unaipata! tuwe waungwana maadili yameporomoka! lakini wanaoshabikia hili shindano wanafanana nalo so hata kama mnasema tunaingilia maisha ya watu tusilikemee hili? simzuii mtu lakini msimamo yangu sipigi kura kwa hili mifano ya vyama na nini sijui mafisadi mnajifariji tuu lakini mioyoni mwenu mnajua maadili yamekiukwa.
 
Back
Top Bottom