Kisa chako ni kama changu tena mimi lilikuwa lishangazi ukweli alikuwa anaishi USA. Tulikuwa tunasalimiana kwa video call usiku nikiwa job tunaongea hata lisaa na watoto wake wa2 wakike wote mmoja mkubwa nadhani ndo alikuwa ananitosha mimi kwa habari ya mbususu.......
Muda ukaenda sana tunaongea nae nami sikuwa na tamaa na niliamini ni mtu sahihi .Basi akanimbia nitume accoun no anipe $26,000 daaah nikasema bahati hii hapa sasa.Kabla sijatuma nilikuwa na m47 ya mkopo kwenye account yangu ya crdb nikamuuliza bro akaniambia mpe yangu ....huyu bro nilikuwa namshirikisha sana hili swala hadi narekodi maongezi yetu namtumia anasema umepata asee.. baada ya kutuma ile no akauliza mbona majina tofauti?
nikamjibu acc yangu inashida kubwa akasema usijari hizo pesa nitatuma pamoja na mizgo mingine..... siku ya kutuma ulivyotoa maelezo ni hivyohivyo sema vitu ni simu3 zote iphone computer 4 (laptop) JBL (radio) nguo vifaa vya michezo na viatu nk yalikuwa mabox2 na hela hizo wakuu kipindi anafunga huo mzigo huku ana record video then akatuma.Alinimbia computer na simu nitawapa wazazi pia na wife.
Nilipata hamasa then akatuma ticket halafu muda sio mrefu akatuma mzigo upo airpot ya huko USA!
Baada y muda akasema nimewasiliana na watu wa huko watakuchaji kama 1.421,000/= kama ushuru hivyo utawapa hiyo hela nikamwambia sawa .....baada ya masaa2 nikatumiwa msg ""Habar bwana ..... tuna pend kukupa taarifa kuwa mzigo wako utafika hapa uwanja wa ndege wa julius k nyerere saa5 usiku hivyo tunakuomba uwe karibu kuja kupokea mzigo huo... "baada ya msg hiyo mzungu wangu naye akanitumia txt umewasiliana nao nikamwambia ndio
.
Basi mzigo ukafika airpot wakanipigia simu nami nikawaambia nipo mkoani hapo anakuja mtu kuuchukua na hiyo hela. Wakakomaa hela haitolewi cash tunaomba ulipe kwa no hii nikawaambia sawa pigeni picha mkiwa na huo mzigo hapo airpot kwa nyerere then nifanye malipo .....wakawa kimya kama lisaa then wakanipigia tena sauti ya mwanamke hapo nimelala na wife anasikia na nilikuwa nimemwambia juu ya neema hii njema wife akasema wee lipa tu uondoe usumbufu. nikamwambia hapana kesho dogo ataenda kuuchukua hapo halafu akifika na kupokea ndo nitalipa.
Baada ya kushindwa kulipia cha ajabu nilipolomoshewa matusi na jianaume linasema usipende vya bure maku wewe mkuyundu wako..Khaaaaaah halafu nika blockiwa chap yani hata mzungu wangu nae akaniblock vilevile
Nikawaaza sana hadi leo sijawahi pata jibu hii connection huyu mzungu alitoa wapi? Ikumbukwe nina uhakika alikuwa anaisha USA kwa 100% maana alisema ana viwanda na kweli alikuwa anapiga video call naona hata siku ananunua simu na hizo vifaa hadi nachagua rangi za nguo yupo USA hata kiwanja cha ndege ni USA!!
Ilikuwa nikiwa night huku job nae yupo kwake viwandani na niliongea na wafanyakazi wake 2 cha ajabu ni huyu mbogo kunitukania hadi ama yangu.Niliumia sana na kupigwa butwaa hapohapo kaka mkubwa nilikaa kimya hadi aliponiuliza vipi kuhusu mzungu wako? nikamwambia tapeli lile. Hadi picha za wazazi wake na clip fupi alinitumia hata mimi nikifanya hivyo na mambo mengine mengi .....Hii connectioni huwa wana toa wapi hawa watu ?
Manyanza Yoda