Ni utapeli au napoteza bahati?

Ni utapeli au napoteza bahati?

Kisa Changu Kiko hivi, Kuna mzungu aliniomba urafiki Facebook baada ya kumkubalia akaniomba namba ya Whatsapp. Tukaanza kuwasiliana ndani ya siku mbili tatu akaahidi kunitumia mzigo ambao ni simu ya iPhone 16.

Yeye anaishi London uingereza na siku aliyotuma mzigo alisema kuwa amekosa ndege inayokuja moja kwa moja Tanzania hivyo akatuma kwenye ndege inayoishia Kenya maana walimwambia kuwa mzigo ukifika wanaweza kufanya delivery uwanja wa ndege ulio karibu (hapahapa East Africa).

Basi bwana yule mzungu akatuma mzigo na akanitumia picha ya mzigo pamoja na risiti na zote Zina majina yangu maana aliniambia nimtumie majina yote matatu na namba ya simu, na akaniambia mzigo utafika Nairobi baada ya masaa 9 na akanisisitiza kuwa niwe Makini na muda kwani mzigo ukishafika watanijulisha na kweli baada ya masaa Tisa (mzigo aliutuma saa 2 usiku saa 11 ukawa umefika Jomo Kenyatta Airport Kenya).

Wale jamaa wa airport wakanipigia wakaniambia kuwa Kuna mzigo wangu wameupokea kutokea uingereza na umeshalipiwa Kila kitu ni Mimi kwenda na kitambulisho Changu tu nikauchukue.

Nikawaambia Mimi sipo Kenya nipo Tanzania Kama wanaweza kuutuma wautume. Kwa sehemu niliyowaambia wakasema inagharimu shilingi 125,000 ili mzigo ufike uwanja wa ndege niliopo.

Wamenionesha na picha ya mzigo kabisa ndio ule uliotumwa Kule uingereza. Sasa najiuliza hii kitu imekaaje? Maana wao wanasema mzungu kalipia mzigo mpaka pale ulipofikia Ila hizo gharama za kuja huku Tanzania ni gharama nyingine kwakuwa mzigo unatakiwa kukatiwa ticket na hiyo ni gharama ya ticket.

Na njia ya malipo wamesema naweza kutumia mpesa au Tigo pesa. Ndo najiuliza hapa nitumie au nakaribia kutapeliwa? Maana Sina uzoefu na upokeaji wa mizigo iliyotumwa kutokea nje ya nchi.

Nawasilisha wakuu. Naombeni ushauri wenu.
Mbongo humwambii kitu kwa mzungu hata ukimwambia ale Mavi ya mzungu atakula tu! Kwamba kuchati nae siku mbili tayari amekupa na iPhone? Mbona huu utapeli wa kitambo sana
 
Kumbe jamiiforum kuna vijana wajinga kiasi hiki?
Wewe mtoa mada umezaliwa wapi?
 
Screenshot_20250126-161241.jpg
 
Nimekutana navyo mara nyingi tu Swahiba...
Hadi kwenye email huko..🤣
Hiyo miujiza ilifanyika enzi za Musa na Wana wa Israeli tena ulikuwa ni msosi tu. Sasa dunia hii ilivyochafuka unapataje free boat?? 🤣🤣🤣
 
Nimepitia coments zote za huu uzi,wengi wanamwambia jamaa anatapeliwa,ila kwa kuwa akili ni nywele kila munu ana zake basi atadhani wanamuonea wivu asipate iphone16 basi nadhani atatuma. Na akituma habari yake itaishia hapo.
 
utapeli huo mwenyewe yame wai nikuta DHL ndo walisanua nilipo enda ofisini kwao
 
Alafu unaweza kuta sio mzungu ni waafrika hawa hawa wanajua kuna Mtu ataingia kingi
Na wazngu pia wapo mkuu,kipind nakaa nyumba za kupanga moro Town Kuna jamaa muuza nguo alipigwa ad alipagawa akaletewa mzungu n jamaa yake wa kalibu yule mzungu anadai alitokea mikum akasema ampe M3 akamletee mizogo ya ngu ya kutosha content 2 na nusu mwamba akaingia kingi kauza ad boda yake katoa na ela ya mtaji wa nguo kampa mzungu baada ya kumpa akimpigia mzungu sim hapatikan na yule mbongo ambae n mwanae wa faida pia hapatikan n mtihan Sana kwakweli
 
Back
Top Bottom