Ni utaratibu gani wa kufuata ili kuanzisha nchi?

Kazanazo

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2023
Posts
7,875
Reaction score
12,665
Nimepata wazo la kijasiliamali la kuanzisha nchi eneo na watu nipo nao ni mimi tu kupata kibali cha kusajili na kupata seat UN ili nianzishe sarafu yangu na mambo mengine ya kiserikali

Naombeni muongozo kwa anaejua nianzie wapi ili kuisajili nchi yangu itambulike kisheria

Nawasilisha
 
Nafikiri ukienda nje ya mipaka ya Dunia yetu hii, yaani nyuma ya safu za barafu za Antarctica, unaweza jitwalia ekari kadhaa na ukaanzisha mji wako. Nafikiri ni kuwahi tu eneo na ukiwa na kikundi cha watu
 
Kisha nchi yake ataipachika jina kama la ile mitaa huwa inaingiliwa na wavamizi wa viwanja majina kama"Tukale wapi,Tukaishi wapi,Ujanja kuwahi,Bora kupata,Shauri zao,Watajua wenyewe,Cha kuokota sio cha kuiba"
 
Mijegeje + wafuasi walio tayari kufa vitani + Kuomba msaada wa nchi kubwa wakufadhili kwa makubaliano wachukue migodi au visima kadhaa vya mafuta

Hao wafadhili hawatakagi vita iishe, wananufaika zaidi mkiwa vitani
 
Haha! Wazo lako limenikumbusha filamu ya Rose Island (2020) ambayo imetokana na matukio ya kweli (based on true story).

Engineer Giorgio Rosa alifanikiwa kujenga kisiwa chake, lakini serikali ya Italy ikaingilia kati japokuwa jamaa alicheza kete zake kwa ustadi mkubwa kwa kujenga kisiwa chake kwenye international waters, sehemu pekee ambayo ilikuwa hakuna nchi yoyote inaweza kumgusa.

Kwa wazo lako ni ngumu kupata ardhi isiyo na mtu/matumizi ili kuanzisha nchi yako.

Ila kuna jamaa, Vít Jedlička, muanzilishi na Rais wa The Free Republic of Liberland, mwaka 2015 alichukua eneo lisilokuwa na mwenyewe (unclaimed land) lililopo mpakani mwa Croatia na Serbia lenye ukubwa wa 7,000,000 m² na kufanikiwa kuunda na kutangaza kuwa eneo hilo ni nchi yake. Mpaka sasa nchi yake ina bendera, sarafu ya kidijitali (cryptocurrency) Liberland Dollar (LLD), na wananchi ambao wanasajiliwa na kupewa pasi za kusafiria (passport), japokuwa bado nchi ya Liberland haijatambulika kama nchi na mwanachama yoyote wa UN.
 
Nenda kwa mwenyekiti akupe barua ya kwenda kuchukua kibali kwa mzee wa nyumba 13 maana cku hizi watu wameongezeka sio kumi tena. Baada ya hapo atakupa barua ya kwenda kwa mwalimu aliyekufundisha civics mwambie akupe notes zote uende nazo hadi hospital iliyo karibu na wewe wakugongee mhuri. Baada ya hapo watakwambia uende mirembe ward no.3 utakutana na mtu hapo amekaa kwene kona atakusainia. Kaz kwisha.
 
Nimepata wazo la kijasiliamali la kuanzisha nchi eneo na watu nipo nao ni mimi tu kupata kibali cha kusajili na kupata seat UN ili nianzishe sarafu yangu na mambo mengine ya kiserikali

Naombeni muongozo kwa anaejua nianzie wapi ili kuisajili nchi yangu itambulike kisheria

Nawasilisha
Utaanzisha wapi Dunia yote inshagombaniwa
 
Mijegeje + wafuasi walio tayari kufa vitani + Kuomba msaada wa nchi kubwa wakufadhili kwa makubaliano wachukue migodi au visima kadhaa vya mafuta

Hao wafadhili hawatakagi vita iishe, wananufaika zaidi mkiwa vitani
Yani kusajili kanchi kako hadi upigane vita?
 
Haha! Wazo lako limenikumbusha filamu ya Rose Island (2020) ambayo imetokana na matukio ya kweli (based on true story).

Engineer Giorgio Rosa alifanikiwa kujenga kisiwa chake, lakini serikali ya Italy ikaingilia kati japokuwa jamaa alicheza kete zake kwa ustadi mkubwa kwa kujenga kisiwa chake kwenye international waters, sehemu pekee ambayo ilikuwa hakuna nchi yoyote inaweza kumgusa.

Kwa wazo lako ni ngumu kupata ardhi isiyo na mtu/matumizi ili kuanzisha nchi yako.

Ila kuna jamaa, Vít Jedlička, muanzilishi na Rais wa The Free Republic of Liberland, mwaka 2015 alichukua eneo lisilokuwa na mwenyewe (unclaimed land) lililopo mpakani mwa Croatia na Serbia lenye ukubwa wa 7,000,000 m² na kufanikiwa kuunda na kutangaza kuwa eneo hilo ni nchi yake. Mpaka sasa nchi yake ina bendera, sarafu ya kidijitali (cryptocurrency) Liberland Dollar (LLD), na wananchi ambao wanasajiliwa na kupewa pasi za kusafiria (passport), japokuwa bado nchi ya Liberland haijatambulika kama nchi na mwanachama yoyote wa UN.
Mimi nataka nchi yangu itambulike kabisa na Umoja wa mataifa na sarafu yangu iwe miongoni mwa sarafu shindani kimataifa nipe muongozo mkuu
 
Jambo la kwanza na la umuhimu na lazima ni kupigana na serikali yako mana hiyo serikali haitoruhusu hilo, hvy inabidi mabavu ili kufanikisha hilo.

Study case: n kama ilivyotokea kwa South Sudan
Sina mpango wa kugawana mali za waarabu Mimi nina eneo langu na watu ninao hapa natafuta kibali tu sijui naanzia wapi
 
Back
Top Bottom