Ahsante sana ndugu yangu. Vipi kwa case ya mtu kuhamia shule nyingine, kwani mtoto huyo kachaguliwa kwenda Ludewa PCB na amesoma shule ya Kata/day wilayani Rorya. Wazazi wake kiuchumi wako vibaya na unaweza ukaona tu jinsi nauli tu itakavyowakamua hawa wazazi ambao waliweza tu kumsomesha mtoto wao shule ya day.
Hakika wazazi wangependa mtoto wao atimize ndoto yake lkn umbali kwao ni tatizo hasa kuhusu gharama za shule. Kwa upande wa Private Schools hawawezi, kwani uchumi wao ni mbovu sana, na ktk upangaji wa shule za serikali ndiyo huyu kijana amejikuta anapelekwa Ulayasi Secondary School iliyoko wilayani Ludewa.
Naombeni ushauri tafadhali kama kuna namna huyu mtoto anaweza akahamia japo shule zilizoko Mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa Combination ya PCB au kama anaweza akabadilsha Combi na kuhamia japo maeneo hayo ya kanda ya Ziwa.
Naomba mwenye kuelewa utaratibu, gharama, na ugumu/urahisi wa jambo hili anisaidie ushauri, kwani nipo mbali kidogo.
Ahsanteni sana.