Pre GE2025 Ni vema CHADEMA wasishupaze shingo itavunjika

Pre GE2025 Ni vema CHADEMA wasishupaze shingo itavunjika

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sijawahi kumuelewa pasikali bora mwasambwa anaeleweka mchumia tumboo..
 
Wewe si unasema tuu kuwa tumeichoka CCM, sisi wenzako ni waandishi wa habari, sio tuu tumesema, bali pia tumeandika sana tuu, CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga! hata uichoke vipi kama hakuna mbadala, tutaendelea kuichagua tuu CCM mwaka hadi mwaka mpaka mbadala upatikane!.
P
hatuichagui ila alichosema nape ndo ukweli wenyewe ccm haiongozi nchi kuchaguliwa bali kwa sababu wao wanaandaa uchaguzi kisha wanajitangaza kuwa wameshinda tunahitaji mabadiliko.
Ni kweli chadema haijajipanga vyema kuing'oa ccm madarakani lakini ni bora chadema kuliko ccm
 
Wasalaam,

Inafahamika wazi nchi hii hakuna vyama vya upinzani zaidi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA). Vyama vingine vyote vinavyojiita vya upinzani ni matawi ya CCM na vimeanzishishwa ili kudhoofisha nguvu za CHADEMA.

Sasa kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa baadae mwaka huu ni vema chadema WASISHIRIKI uchaguzi huu ambao unasimiwa na makada wa CCM ambao wameshaahidi tena hadharani kwamba hakuna kata itakayoenda upinzani.

Nawashauri CHADEMA kama kweli wapo kwa ajili ya kulikomboa taifa hili dhidi ya mkoloni mweusi CCM basi wadai Tume Huru ya kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa na sio kuwaachia kina Mchengerwa wafanye hujuma kama walivyomuahidi mwenyekiti wao ambae ndie mteuzi wa wasimamizi wa uchaguzi huo.

Angalizo: Endapo CHADEMA watashikiriki uchaguzi huu katika MAZINGIRA haya batili basi watanzania wenye kujitambua wataamini nchi hii hakuna chama cha upinzani wote ni ccmB na mnalamba asali na kusaliti matumaini ya watanganyika kwenu.

Ova.
Ushauri mbovu na wa hovyo...

Yote yanapaswa kufanyika kwa wakati mmoja; kushiriki uchaguzi na kudai katiba mpya...

Ni kweli mazingira na uwanja wa uchaguzi si fair na siyo sawa kwa vyama vya siasa shiriki vyote...

Mazingira na dalili zote zinaonesha kuwa CCM, chama kinachoongoza serikali sasa na ambacho makada wake licha ya kwamba ni washiriki wa uchaguzi, pia ndio watunga kanuni na ni marefa/waamuzi wa uchaguzi wote...

Pamoja na mazingira haya magumu, lazima tupambane nao ndani ya mazingira hayahaya kwa kutumia njia zote halali ikiwemo mahakama hata kama haiaminiki kwa 100%....

Ndiyo maana kuna kesi inaendelea kupinga TAMISEMI kusimamia uchaguzi huu. Au hujui...?

HAKUNA KUSUSA. NI KUPAMBANA NAO HADI KIELEWEKE....!!
 
Ni kweli chadema haijajipanga vyema kuing'oa ccm madarakani lakini ni bora chadema kuliko ccm
Utawasaidia sana wapiga kura ukiusema huo ubora wa Chadema, ili wapiga kura tuwachague Chadema tuwakabidhi Ikulu yetu.
P
 
Njaa na mapambano haviendi pamoja.

Chadema wana njaa na wakati huo huo wanatakiwa kupambana. Unadhani inawezekana kususia uchaguzi?
 
CHADEMA ni nini au ni nani?

Siyo itikadi na imani ya wafuasi?
Siyo watu ambao na wao wanatakiwa kula, kusomesha na kuishi leo?
Siyo mimi na wewe?

Waache siasa ili wafanye nini? Wakiacha kwa ajili ya mabadiliko ya baadaye je leo itakuwaje?

Lazima tuishi leo, sasa, tuendelee kudai tume huru, katiba, lakini tuendelee kuminyana vikali na ccm leo na sasa na hata milele.

Ebooo
 
Back
Top Bottom